Friday, May 29, 2015

Ni Diamond Platnumz tena kwenye Headlines time hii kamshirikisha Mr. Flavour…

XXXXNi kolabo nyingine kutoka kwa Mtanzania Diamond Platnumz ambayo hii kamshirikisha mkali kutoka Nigeria Mr.Flavour wimbo unaitwa Nana,video imefanywa na GodFather mtu wangu.
Diamond Platnumz ametumia dakika hizi tatu kumuimbia mrembo aliye mbele ya macho yake,unaweza kumuandikia chochote hapa Diamond kisha baadae atapita na kusoma comment yako mtu wangu.
XX2
U

KIGOMA SHIRIKISHO LA ELIMU YA JUU MKOWA WA KIGOM 


HIZI NI BAADHI YA PICHA ZA WANASHIRISHO ZIONE HAPO

 








Hii ndiyo shughuli ya Lowassa kesho.. Uwanja wa Sheik Amri Abeid utatapika kesho ...Je! Hao wana CCM wengine wanaotarajia kutangaza nia wana nguvu ya kutosha? Makongoro, Wasira, Membe, Mwigulu... Mkombozi wenu ni CHIMWAGA (NEC) tu..

Je wewe upo Team Gani?

Sepp Blatter ametangazwa mshindi wa kiti cha urais wa Shirikisho la Soka Duniaani FIFA kwa mara ya 5 mfululizo baada ya kupata kura 133 dhidi ya 73 za mpinzani wake Prince Ali bin Al-Hussein.
Katika hotuba yake baada ya kutangazwa msindi, Blatter amesema anajivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha uongozi wake, ikiwemo kuanzishwa kwa mchezo wa soka la ufukweni (Beach Soccer).

“Tumefanikiwa kuanzisha Beach Soccer na sasa mchezo huo unachezwa kote duniani”
Akizungumzia umri wake, Blatter mwenye umri wa miaka 79 amesema kuwa umri mkubwa hauwezi kumzuia mtu kutimiza majukumu yake, na hivyo kwake umri siyo tatizo.
Tanzania imewakilishwa na Rais wa TFF Jamal Malinzi ambaye tayari alikwisha tangaza msimamo wa Tanzania kuwa ina muunga mkono Sepp Blatter, kwa maana hiyo bila shaka kura yake ni miongoni mwa kura 133 alizopata Blatter.

Kwa upande wa mpinzani wake Prince Ali bin Al-Hussein amekubali matokeo na kutangaza kujitoa baada ya awamu ya kwanza ya upigaji kura

Je, uonavyo wewe, Blatter anastahili kuendelea kuongoza shirikisho hilo ?

Tanzania Kuendelea Kupokea Wakimbizi wa Burundi

Mpekuzi blog

TANZANIA imetangaza kuendelea kupokea wakimbizi wanaoingia nchini kutoka Burundi kutokana na kuendelea kwa machafuko nchini humo huku waandamanaji wakipambana na polisi kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunzinza kugombea urais kwa muhula wa tatu.
 
Akizungumza  katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kabla ya kuanza safari ya kukagua kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Wilayani Kasulu jana, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe alisema uamuzi huo unalenga kutoa nafasi ya wakimbizi hao kupata mahitaji ya msingi.
 
Waziri Chikawe alisema wakimbizi wana haki ya kulindwa na kuthaminiwa kama raia wengine kwa hivyo uamuzi wa Serikali kutoa nafasi zaidi kwa wakimbizi nchini una nia ya kutoa nafasi zaidi ili kupata mahitaji yao ya msingi ikiwa ni pamoja na misaada mbalimbali ya binadamu kupitia mashirika mbalimbali.
 
 “Kama nchi tumeona ni vema kuendelea kuwapokea, hivyo tumetoa nafasi ya kuendelea kuwapokea wakimbizi hawa kutoka nchini Burundi mpaka hapo hali ya usalama nchini mwao itakapoimarika,” alisema Chikawe.
 
Waziri Chikawe pia aliyaomba mashirika mbalimbali ya kimataifa kusaidia wakimbizi hao wanaoendelea kumiminika nchini kwa wingi kusaidiana na serikali ili kuwapa huduma za malazi na chakula.
 
  Mratibu Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez alisema mpaka sasa hali ya siasa  Burundi inatia shaka kwa kuwa inaweza kusababisha ongezeko kubwa la wakimbizi Tanzania.
 
Alisema Tanzania ni nchi ya mfano wa kuigwa kwa namna inavyoshughulikia wakimbizi ikiwa ni pamoja na kuwapokea hiyvo umoja wa mataifa unaungana na nia ya Serikali ya Tanzania kuwasaidia wakimbizi hao.
 
Alisema kutokana na kuendelea kupokea idadi kubwa ya wakimbizi, kambi ya Nyarugusu imeendelea kuelemewa na wakimbizi hivyo kuliomba shirika la Umoja wa Mataifa kusaidia uwezekano wa kuongeza kambi nyingine kwa ajili ya wakimbizi hao.

Meya wa Jiji la Mbeya na Mbunge Joseph Mbilinyi ( CHADEMA) Waingia Katika VITA Ya Maneno.........Kisa na Mkasa ni Jimbo la Mbeya Kugawanywa

Mpekuzi blog

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga, amesema  hana sababu ya  kuendelea kujibizana na Mbunge wa Mbeya Mjini,  Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Chadema), kwani amekuwa akimpa changamoto za kiutendaji ambazo zimemfanya kufanya kazi kwa ufanisi.
 
Amesema, mbunge huyo anaapswa kusubiri kubali cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ili aweze kutumia vema jukwaa la kisiasa kuliko ilivyo sasa anavyotumia Bunge kuwachafua watu wengine.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Mbeya, Meya Kapunga,  alitumia nafasi hiyo kutoa ufafanuzi kuhusu hali halisi ya utendaji kazi wake uliokuwa umezungukwa na majungu, chuki na fitina zisizokuwa na msingi zinazoendelea kutolewa na Mbunge ‘Sugu’  ambaye alimfananisha sawa na chipukizi wa kisiasa.
 
“Leo (jana),  asubuhi nimemsikia Sugu, akizungumza bungeni kuhusu ugawaji wa Jimbo la Mbeya Mjini na kunitaja mimi ni miongoni mwa viongozi wanaoshinikiza kugawanywa kwa jimbo hili, wala sikatai ni kweli kwani mchakato huu wa kuligawa jimbo hili niwa muda mrefu kabla ya Sugu kuingia ulingoni,” alisema Kapunga
 
Alisema, mchakato wa kuligawa jimbo hilo, ulianza mwaka 2008 ukiwa chini ya Mbunge  Mpesya hivyo yeye kama Meya ni jukumu lake kulisemea hilo kama mtendaji wa halmashauri.
 
“Hapa kosa langu nini mpaka Sugu kunisema bungeni, kwanza nimeona ni mtoto anayezoea tabia mbaya, kukaa kila saa ananisema bungeni anaonyesha ni jinsi gani asivyokomaa kisiasa,” alisema
 
Alisema, Sugu ni mjumbe wa vikao vya kiutendaji vya halmashauri ana nafasi kubwa ya kufika na kuyazungumzia hayo tatizo linalomsumbua ni upeo wake mdogo wa kufikiri hivyo kujiaminisha kwambajimbo la Mbeya ni mali yake.

Alisema,  Mbeya ni mali ya  wananchi, si la ukoo na kitendo cha kuwaza jimbo ni mali yake ni ujinga,  yeye atabaki kuwa kwenye orodha ya wabunge wa ajaabu ambao kila siku kazi yake ni kumuwaza Kapunga badala ya kusimama na hoja.
 
“Mimi ninamsubili huku kwa wananchi, sasa ngoja nimuache tu aendelee na utoto na jambo la kumsikitikia ni kwamba mpaka leo anaamini akili za wanambea wa miaka mitano iliyopita ziko palepale,” alisema

Mbunge ‘Bwege’ apata Mpinzani Kilwa Kusini


JOTO la Uchaguzi ndani ya Chama cha Wananchi (CUF), limezidi kupanda huku Mbunge wa Kilwa Kusini, Suleman Bungara ‘Bwege’ (CUF), amepata mpinzani ndani ya chama hicho.
 
Pamoja na nguvu na umaarufu aliona mbunge huyo, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mohamedi Taher Abubakari, amejitosa kuwania ubunge katika jimbo hilo.
 
Mohamedi  alitangaza nia hiyo kwenye  mkutano na waandishi wa habari  jana mjini mjini Lindi, alisema ametafakari kwa kina na kuona sasa ni wakati muafaka kwake kuwania ubunge ili kuweza kuleta ukombozi wa kweli kwa wananchi wa Kilwa.
 
 “Nimetafakari  na kutokana na maelekezo ya chama change, nimejipima na nimetazama hali halisi ya maendeleo na kero ya za huduma za kijamii bado ni mbovu  jambo ambalo kwa bahati mbaya jimbo hili linaongozwa na Mbunge  wa CUF,” alisema Mohamedi.

Alisema kuwa uamuzi  wa kuomba nafasi hiyo umetokana na shinikizo kutoka kwa wananchi wa manispaa yna jimbo la Kilwa Kusini wa kumtaka achukue fomu ya kuwania ubunge.