Friday, May 29, 2015

Mbunge ‘Bwege’ apata Mpinzani Kilwa Kusini


JOTO la Uchaguzi ndani ya Chama cha Wananchi (CUF), limezidi kupanda huku Mbunge wa Kilwa Kusini, Suleman Bungara ‘Bwege’ (CUF), amepata mpinzani ndani ya chama hicho.
 
Pamoja na nguvu na umaarufu aliona mbunge huyo, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mohamedi Taher Abubakari, amejitosa kuwania ubunge katika jimbo hilo.
 
Mohamedi  alitangaza nia hiyo kwenye  mkutano na waandishi wa habari  jana mjini mjini Lindi, alisema ametafakari kwa kina na kuona sasa ni wakati muafaka kwake kuwania ubunge ili kuweza kuleta ukombozi wa kweli kwa wananchi wa Kilwa.
 
 “Nimetafakari  na kutokana na maelekezo ya chama change, nimejipima na nimetazama hali halisi ya maendeleo na kero ya za huduma za kijamii bado ni mbovu  jambo ambalo kwa bahati mbaya jimbo hili linaongozwa na Mbunge  wa CUF,” alisema Mohamedi.

Alisema kuwa uamuzi  wa kuomba nafasi hiyo umetokana na shinikizo kutoka kwa wananchi wa manispaa yna jimbo la Kilwa Kusini wa kumtaka achukue fomu ya kuwania ubunge.

No comments:

Post a Comment