kigoma tunaamini sisi sote ni wazalendo wa ukweli basi pata habari zote hapa kwa blog yetu muhimu na pendwa kwa mkoa wa KIGOMA - TANZANIA ENTERTAINMENT News,Politics and other basi unguna na kijana mwenzako RASHID HAMZA MAARUFU KWA JINA LA RD PRO DOGO 'R' SIMU NAMBA 0752987701 PAMOJA TUNAJENGA NCHI YETU NA TUTASHINDA
Tuesday, November 28, 2017
Friday, November 24, 2017
Kafulila atua rasmi CCM na Kukabidhiwa Kadi
Baada ya kutangaza kujivua uanachama wa CHADEMA siku ya Jumatano, David Kafulila jana amekabidhiwa kadi ya CCM.
Kafulila
alikabidhiwa kadi ya CCM na Katibu Mwenezi wa CCM, ndg Humphrey
Polepole katika mkutano wa kumnadi mgombea wa udiwani wa chama hicho,
Kata ya Mbweni jijini Dar es salaam
Hapo
awali Kafulila aliwahi kuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na
Maendelo kisha kufuzwa baadae akajiunga na Chama cha NCCR Mageuzi ambapo
alifanikiwa kuwa Mbunge wa Kigoma Kusini mwaka 2010-2015 na baadaye
kurudi tena Chadema 2016 na hapo juzi jumatano alitangaza kukihama chama
hicho kwa madai upinzani hauna nia ya kupambana na ufisadi.
Kwa
upande wa mkewe ambaye ni Mbunge Viti Maalumu kupitia chama cha
CHADEMA,Jesca Kishoa juzi wakati akizungumza na wanahabari alipingana na
kauli ya mumewe na kusema kwamba, mumewe anapaswa kusema ukweli na
kwamba sababu alizozisema sizo zilizomuondoa ndani ya chama hicho huku
akiongeza kwamba mume wake hana msimamo.
Kafulila
amekabidhiwa kadi hiyo ya CCM ikiwa imebaki siku moja kabla ya
kuhitimishwa kwa kampeni za uchaguzi wa marudio ya nafasi za udiwani kwa
Kata 43 ndani ya Tanzania
Thursday, November 23, 2017
Breaking News: TANZIA: Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama(CCM) afariki dunia
Mchambuzi Huru imepata uthibitisho wa taarifa za kifo cha Mhe. Gama ambacho kinadaiwa kutokea muda wa Saa 6 kuelekea Saa 7 usiku wa kuamkia leo.Amefariki akiwa mbunge wa Songea Mjini na amefariki dunia usiku wa kuamkia leo hii Songea katika Hospitali ya Peramiho.
Gama amewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Muheza, Nachingwea, Newala, Mbeya na Ilala. Vilevile amewahi kuwa mkuu wa mkoa Kilimanjaro.
Inadaiwa marehemu Gama alianguka nyumbani kwake saa saba usiku juzi huko Likuyu; akapooza upande wa kushoto akawa hajitambui kabisa na akapelekwa Hospitali ya Peramiho ambako aliwekewa mashine za kumsaidia kupumua.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali pema peponi
Mke wa Kafulila Atoa ya Moyoni Uamuzi wa Mumewe Kuikimbia CHADEMA
Mke wa aliyewahi kuwa mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila, Jesca Kishoa, amemtaja mumewe kuwa ni mtu aliyeingia kundi la wanasiasa wasio na msimamo.Kishoya amesema wakati wote mumewe amekuwa na msimamo usioyumba lakini anashangazwa kaingia katika mtego mbovu.
"Bado naamini kuwa Chadema ni mahali sahihi kabisa ambapo siwezi kufikiri siku moja nitatoka, hivyo siyumbi kwa hilo na wanaonipigia simu watambue hilo," amesema Kishoya
Amesema taarifa za mumewe kujiondoa Chadema amezipata kupitia vyombo vya habari akiwa Dodoma kwenye kampeni za udiwani lakini alimpigia wakazungumza sana na bado hakumpa sababu zilizoshiba za kuondoka kwake.
Hata hivyo amepinga madai ya Kafulila kuwa anaondoka upinzani kwa sababu ya upinzani kushindwa kusimamia ajenda ya ufisadi badala yake akasema ana mambo yake.
"Wanasiasa ambao hawana misimamo ndiyo husingizia vitu hivyo, siamini kama maneno yale yalitoka rohoni mwake, CCM siyo mahali sahihi kwa kuzungumzia mambo ya ufisadi hata kidogo, "
Mbuge huyo amesema wakati wote katika maisha yao mumewe amekuwa ni muumini mzuri wa kuhubiri habari za ufisadi ikiwemo pale alipotoa maisha yake kuhusu sakata la Escrow.
Kafulila: "Ndoa Yangu Haihusiani na Siasa ilifungwa Kanisani na Sio kwa Mwenyekiti wa Chama"
David Kafulila ambaye hapo jana amekihama chama cha CHADEMA, amesema suala la mke wake kuridhia au kutoridhia kwa yeye kuhama chama wakati yeye ni Mbunge wa chama hiko, ni suala ambalo halihusiani na ndoa yao.Kafulila ameyasema hayo leo na kueleza kwamba linapokuja suala la ndoa hapo ndio huwa lazima wafikie makubaliano, lakini ikija suala la kisiasa kila mtu ana uamuzi wake ambao hawaingiliani kwani ndoa yao ilifngwa kanisani na sio kwenye chama.
“Haya ni maamuzi ya kisisasa, sisi ndoa yetu ilifungwa kanisani haikufungwa kwa mwenyekiti wa chama au kwenye chama, kwa hiyo ndoa ni jambo jingine na harakati ni mjambo jingine, yeye ni mke wangu lakini haimaanishi tunakubaliana kwenye kila kitu, tunakubaliana kwenye mambo ya ndoa, kwenye siasa kila mtu anaweza akatazama jinsi anavyotazama yeye na sio shida”, amesema Kafulila.
Hivi sasa kumekuwa na mvutano kati ya wanandoa hao baada ya Kafulila kuhama CHADEMA, huku mke wake akisema hakuwa na taarifa zozote, na hata hizo sababu zake za kuhama hazina ukweli na kumtaka aweke wazi sababu rasmi za kufanya hivyo
Mhasibu feki atiwa mbaroni kwa wizi wa Tsh. 873,000
Na Nathaniel Limu, Singida
Mhasibu
wa hospitali ya mkoa mjini Singida aliyeachishwa kazi kwa kosa la
kumiliki vyeti feki, Edith Talasi (49) mkazi wa Minga,anashikiliwa na
jeshi la polisi kwa tuhuma ya kuvunja milango ya ofisi yake ya zamani na
kuiba shilingi 873,000 taslimu, kwa kutumia funguo bandia.
Talasi
ambaye imelelezwa kwamba alifanya kazi hospitalini hapo kwa muda na
baadaye alirejeshwa kwenye kituo chake cha kazi manispaa ya
Singida,kwenye wizi huo, alimshirikisha mlinzi wake wa nyumba ya kulala
wageni Nandau, Antony Felix (51).Mlinzi huyo naye anashikiliwa na
polisi.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani
hapa, ACP Debora Magiligimba, alisema tukio hilo limetendeka Novemba, 21
saa 6.30 usiku huko katika hospitali ya mkoa mjini hapa.
Alisema
siku ya tukio muuguzi wa zamu Shamir Omari (27) akitokea maeneo ya
mapokezi akielekea wodini, alimwona mtu akiwa amesimama karibu na ofisi
ya mhasibu, alisimama akamsalimia na mtu huyo aliondoka.
“Muuguzi
huyo aliamini kuwa mtu aliyemwona,huenda alikuwa mgonjwa au mtu
aliyeleta mgonjwa hospitalini.Lakini aliporudi,alimwona mtu yule yule
amerudi eneo lile lile, kitendo kilichopelekea amshuku kuwa sio mtu
mzuri,” alisema kamanda huyo.
Alisema
muuguzi huyo baada ya kumtilia shaka mtu huyo, alitoa taarifa kwa
mlinzi wa zamu wa hospitali hiyo, Abubakari Jumanne,ambaye alimweka
chini ya ulinzi mtu huyo.
ACP
Magiligimba alisema hata hivyo mtu huyo alijitetea kuwa amefika
hospitalini hapo, kwa ajili kuchoma sindano na kuonyesha dawa ya unga na
kichanganyio chake.
“Wakati
wanaendelea na mahojiano hayo,waliona makufuli mawili ya mlango wa
nje/grili yapo chini na mlango huo wa chuma upo wazi. Mtuhumiwa mlinzi
Antony alieleza kuwa bosi wake (mtuhumiwa Edith) kwa wakati huo,alikuwa
ndani ya ofisi ya mhasibu amejifungia ndani,” alisema.
Akifafanua
alisema jeshi la polisi baada ya kupata taarifa ya wizi huo, liliweza
kufika eneo la tukio na kukuta mlango wa ndani ukiwa umefungwa kwa
ndani.
“Walipoamuru
mhasibu afungue mlango huo kwa kutumia funguo zake,walimkuta mtuhumiwa
(Edith) akiwa amejibanza kwenye kona ya mlango na watumishi wa hospitali
hiyo, waliweza kumtambua. Alipohojiwa ameingiaje humo ndani,alionyesha
funguo saba (07) na zilipojaribiwa ziliweza kufungua milango yote ya
ofisi ya mhasibu,” alisema Magiligimba.
Alisema
pamoja na wizi huo wa shilingi 873,000,imeelezwa kwamba aprili mwaka
huu,wahasibu wa hospitali hiyo,walibaini upotevu wa shilingi
1,800,000.Oktoba mwaka huu,pia walibaini upotevu wa shilingi 3,600,000.
Kaimu
mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. David Mwasita,amekiri kutokea
upotevu huo lakini wahasibu katika wakati huo,waliweza kuziba upotevu
huo, kwa fedha zao za mishahara.
Ameeleza
kuwa wahasibu hao walilazimika kutoa fedha zao binafsi, na wasingeweza
kutoa taarifa ya upotevu huo, kwa vile milango na kasiki, ilikuwa
imefungwa kama kawaida.
ACP
Magiligimba amesema kwa sasa wanaendelea kuwahoji watuhumiwa hao na
baada ya kumalizika kwa mahojiano hayo,watuhumiwa watafikishwa
mahakamani kujibu tuhuma inayowakabili.
GodBless Lema Amtaka Kafulila Amshauri Mkewe Naye Ajiondoe CHADEMA
Mbunge
wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA Godbless Lema, amefunguka kuhusu
kitendo cha David Kafulila kuhama CHADEMA na kusema ana amini atamshauri
mke wake naye afuate nyayo zake.
Kwenye
ukurasa wake wa twiter Godbless Lema ameandika ujumbe akisema Kafulila
ni rafiki yake wa karibu, lakini kwa namna alivyoamua hana shaka
atamshauri mke wake ambaye ni mbunge kupitia chama cha CHADEMA, kufanya
kama yale aliyoyafanya.
"David
Kafulila ni rafiki yangu, nafikiri kwa namna hii alivyoamua ataweza
bila shaka kumshauri Mbunge wa Chadema, Jesca Kishoa (mke wake) kufikiri
kama yeye, hii inaweza kusaidia maoni yake juu ya uamuzi aliouchukua
leo na kuthibitisha ukweli huu kama hupo", ameandika Godbless Lema.
Jana
David Kafulila ametangaza kukihama chama cha CHADEMA akidai vyama vya
upinzani havina nia ya kupambana dhidi ya ufisadi, lakini mke wake Jesca
Kishoa ambaye ni mbunge wa viti maalum kupitia CHADEMA bado
hajazungumza chochote.
Wednesday, November 22, 2017
Zanzibar na Njema Kwa Wageni na Wenyeji wa Zanzibar.
Watalii wanaofika kutembelea Zanzibar hupata fursa za kutembelea katika
maeneo mbalimbali ya historia ya Zanzibar katika maeneo mbalimbali ya
Visiwa hivi kama walivyokutwa Watalii hawa wakiwa katika maeneo ya mji
mkongwe wa Unguja katika mitaa ya shangani wakipiga picha kwa ajili ya
kumbukumbu jengo la Marcury shangani.
Kaim Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Wa Chama Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamidu shaka muda Mchache uliopita alikuwa akiongea na waandishi wa Habari,akielezea mambo mbalimbali juu ya Umoja huo wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Kupitia mitandao mbalimbali ya Kijamii kama Facebook na Instagram katika Page zao za Uvccm Taifa.
Waziri Mwijage Aweka Jiwe la Msingi Katika Kiwanda cha Usambazaji Vifaa vya Ujenzi
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijange, leo ameweka jiwe la msingi eneo la Tabata-Matumbi jijini Dar es Salaam ambapo kiwanda hicho kitakuwa kikisambaza vifaa vya ujenzi.Akizungumza katika hafla hiyo, Mwijage ameipongeza kampuni ya CNBM ya China kwa namna ambavyo imedhamiria kuwekeza hapa nchini kwa kuanzisha kituo cha usambazaji wa vifaa hivyo.
Alisema Tanzania na China zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na serikali ya Tanzania itaendelea kuwaunga mkono wawekezaji wenye nia njema kwa serikali hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda.
Aliwapongeza pia watu wote wenye nia ya kuwekeza hapa nchini katika miradi mbalimbali ya viwanda kwa upande wa mazao kama vile muhogo, zao ambalo sasa ni muhimu na lenye kuweza hata kuuzika nje ya nchi.
Alisisiza kwamba kituo hicho kitawasaidia Watanzania kujipatia ajira na kuongeza ufanisi kwa vijana nchini kwa kunufaika na kituo hicho.
Naye Balozi mpya wa China hapa nchini, Bi Wang Ke, alimpongeza Mwenyekiti wa kampuni hiyo ya CNBM, Song Zhiping, kwa kuanzisha kituo hicho ambacho kitakuwa muhimu
Makamu wa Rais wa Zimbabwe Akataa Kurudi Nyumbani
Wakati Emmerson Mnangagwa alipofutwa kazi wiki mbili zilizopita hakuwa makamu wa rais wa pekee nchini ZimbabwePhelekezela Mphoko ni makamu wa rais mwengine ambaye anajulikana kwa kumuunga mkono mkewe rais Mugabe na kulingana na sheria anapaswa kumrithi Mugabe.
Hatahivyo chama cha Zanu PF kimsema kuwa Mnangagwa ataapishwa kufuatia uamuzi uliochukuliwa na kamati yake kuu siku ya Jumapili.
Bwana Mphoko alikuwa ameondoka katika taifa hilo wakati Jeshi lilipochukua mamlaka wiki moja iliopita, na kulingana na gazeti la NewsDay hajarudi nyumbani kwa kuwa anahofia kukamatwa.
Gazeti hilo limenukuu duru akisema kuwa amebadilisha mipango yake ya usafiri.
Alitarajiwa kurudi nchini zimbabwe kufikia siku ya Ijumaa , kutoka Tokyo Japan.
Lakini duru zimesema kuwa anataka tiketi zake za usafiri kubadilishwa ili aelekee Zambia au Msumbiji .
Anajua anaogopa kukamatwa kwa sababu anatakikana kwa kuzuia haki na kufanya ufisadi.
Davina Awatetea Viben Ten " Mapenzi Hayachagui Umri"
LICHA ya wengi kuwaponda wanawake wenye umri mkubwa wanaokuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume wadogo kiumri ‘viben’ten’, staa wa filamu za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ amewatetea kwa kusema siyo vibaya kwani mapenzi hayana umri.Akipiga stori na Za Motomoto News, Davina alisema licha ya kutowahi kuwa na kiben’ten, haoni tatizo kwa wanaokuwa na uhusiano na wanaume hao wadogo kwa kuwa siku zote mapenzi hayachagui umri, dini wala kabila bali mtu hujikuta amependa tu.
“Sijawahi kuwa na kiben’ten huwa naona ni bora kuwa na mtu ambaye tunalingana kiumri au amenizidi kidogo, wanawake wanaokuwa na wanaume hao wadogo siwezi kuwalaumu au kuwacheka kwa sababu mapenzi ni kitu ambacho hakizuiliki wala hakichagui,” alisema Davina.
Dr. Luis Shika kalipwa tena kuuza sura, sasa ni kwenye hii video ya Bongofleva (+video)
Director Khalfan ambae ndio fundi wa hiyo video ameithibitishia AyoTV na millardayo.com kwamba Dr. Luis Shika amelipwa ili atokee kwenye hiyo video ya Msanii wa Bongofleva ambae alisema hawezi kumtaja kwa sasa.
Hili linakua dili la pili kwa Dr. Luis Shika kulipwa ili kuuza sura ambapo dili la kwanza lilikua ni tangazo la SOKA BET ambako pia alilipwa na kampuni hiyo ilithibitisha kufanya hivyo
Paul Makonda Aibuka Ofisi za Clouds Media Kuwapa Pole
Clouds Wameandika haya Baada ya Paul Makonda Kuwatembelea Kuwapa Pole:
...
"Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam, ikiongozwa na RC Paul Makonda wamefika hapa #Mjengoni - #CloudsMediaGroup kutupa pole na kujionea athari zilizosababishwa na moto uliozuka jana asubuhi katika Ofisi zetu hapa Mikocheni. .
.
Tunashukuru kwa yote, tuko salama"
Picha za Irene Uwoya kwenye kaburi la Ndikumana
Mume wa zamani wa Mwigizaji Irene Uwoya, Hamad Ndikumana
alifariki ghafla wiki iliyopita huko Rwanda sekunde chache baada ya
kuomba soda ya baridi na kunywa ambapo Irene alifanikiwa kusafiri mpaka
kwao kwenda kutoa pole kwa familia.
Kwenye hizi picha hapa chini anaonekana akiwa nyumbani kwa kina Ndikumana na ndugu zake na juu ya kaburi la Ndikumana pia ambapo chini mwishoni kuna video fupi ikimuonyesha Irene akipewa baraka na Baba Mzazi wa Ndikumana
Baada ya taarifa hizo Irene Uwoya alifunga safari baadae na kwenda kutoa pole kwa familia ya Ndikumana ambapo ameonekana akiwa na Mtoto wao Krissh juu ya kaburi la Ndikumana na kuandika “My trust is in you …R.I.P baba krissh”
Kwenye hizi picha hapa chini anaonekana akiwa nyumbani kwa kina Ndikumana na ndugu zake na juu ya kaburi la Ndikumana pia ambapo chini mwishoni kuna video fupi ikimuonyesha Irene akipewa baraka na Baba Mzazi wa Ndikumana
Baada ya taarifa hizo Irene Uwoya alifunga safari baadae na kwenda kutoa pole kwa familia ya Ndikumana ambapo ameonekana akiwa na Mtoto wao Krissh juu ya kaburi la Ndikumana na kuandika “My trust is in you …R.I.P baba krissh”
Tuesday, November 21, 2017
Isome Hapa Barua ya Kujiuzulu Aliyoandika Rais Robert Mugabe
Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe, Robert Mugabe, jana alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo baada ya kuongoza taifa hilo kwa miaka 37 tangu lilipopata uhuru mwaka 1980.Mugabe katika barua aliyoiandika kwenda wa Spika wa Bunge, alisema uamuzi huo ni wa kwake binafsi na kwamba hajashinikizwa na mtu yeyote.
Katika barua yake ya kujiuzulu, Mugabe aliiandika jana Novemba 21 na kuielekeza kwa Spika wa Bunge, Jacob Mudenda.
Mugabe aliandika kuwa, kwa mujibu wa kufungu cha 90(1) cha Katiba ya Zimbabwe marekebisho ya namba 20 ya mwaka 2013.
“Kufuatia mazungumzo yangu na Spika wa Bunge, Wakili Jacob Mudenda majira ya saa 7:53 mchana, Novemba 21, 2017 kuhusu kutangaza kujiuzulu kama Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mimi Robert Gabriel Mugabe, kwa mujibu wa kifungu cha 90(1) cha Katiba ya Zimbabwe natangaza rasmi kujiuzulu kwangu kama Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe mara moja.”
“Uamuzi wa kujiuzulu ni wangu kwa chama, na nimefanya hivi kwa maslahi ya watu wa Zimbabwe na nia yangu ya kuona makabidhiano ya madaraka yenye amani ambayo yatashikilia amani, utulivu na umoja wa taifa.”
Aidha, Rais Mugabe alisema, “Tafadhali utangazie umma kuhusu kujiuzulu kwangu haraka iwezekanavyo kama inavyotakiwa na kifungu cha 96(1) cha Katiba ya Jamhuri ya Zimbabwe.
“Wako Mwaminifu, Robert Gabriel Zimbabwe, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe,” alihitimisha Rais Mugabe.
Kufuatia kujiuzulu kwa Mugabe, wananchi katika Mji Mkuu wa Zimbabwe, Harare walitoka katika mitaa mbalimbali na kushangilia huku wakisema kuwa ni awamu mpya kwa Zimbabwe sasa kuendelea kiuchumi.
RIWAYA YA MATESO YA MAMA
Wapendwa Wafuatiliaji wa Blog yetu Kuanzia siku ya Ijumaa ya Tarehe 24/11/2017 Tutawaletea Riwaya ya Mateso ya Mama na itakuwa inendelea kwa kila siku hivyo Mwambie Rafiki,Jirani,na Mtu wako wa karibu kuwa Asikose kufuatilia kwani ni Riwaya nzuri sana.Don't Miss
Kutoka kwa Mtunzi wetu Makini RD
MASHINJI ATOA NENO KWA ALIYEKUWA KIONGOZI WA BAVICHA KATAMBI AMBAE SASA AMEHAMIA CCM
Katibu Mkuu wa
Chadema, Dk Vincent Mashinji amesema chama hakina mgogoro na aliyekuwa
Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi ambaye ametangaza kujiunga na
CCM kwa kuwa ni haki ya Kikatiba.
Akizungumza na
Mwananchi Jana Jumanne baada ya Katambi kuhamia CCM, Dk Mashinji, “sisi
kama chama msimamo wetu tuliuweka tangu madiwani walivyoanza kuondoka,
tukaweka msimamo wazi kwamba, suala la mtu kuondoka kwenye chama au
kubaki ni suala la Katiba ya nchi ambayo inampa mtu uhuru wa kuhama na
kwenda kwenye chama anachotakana.”
Amesema kuwa haoni sababu ya kumzuia mtu kuondoka kwa kuwa mtu anapoamua kwenda sehemu yoyote anakuwa na matarajio.
Pia, Dk Mashinji
amesema anamtakia heri (Katambi) na kuwataka CCM kumtumia katika sehemu
ambavyo wanaona anafaa kutumika kwa faida ya Watanzania wote.
“Hatuna mgogoro
wowote na kimsingi mimi nimtakie tu heri (Katambi) na wakipenda (CCM)
wamtumie kwenye eneo watakaloona anafaa kutumika kwa faida ya Watanzania
wote,” amesema
Hata Hivyo, Dk Mashinji amesema kuwa walikuwa wanamuandaa Katambi asaidie chama hicho kwenye kitengo cha sheria.
“Alikuwa
anamalizia masomo yake ili awe wakili na tulikuwa tumeshaanza kumuandaa
ili atusaidie kwenye kitengo cha sheria ndani ya chama,”
Katambi ametangaza
leo kujiunga na CCM mbele ya Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC)
unaofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Edward Lowassa Afungukia Kuhamia CCM....Afunguka Haya
Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema hana mpango wa kurejea CCM kama ambavyo taarifa zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.Lowassa alisema jana Jumanne kuwa amepata taarifa za uvumi unaosambazwa kuwa kuna watu amewatuma kuomba arudi CCM jambo ambalo ni uongo.
"Huu ni uongo wa kutunga, wamekuwa wakitunga vitu vingi juu yangu, mimi sina mpango wa kurejea CCM," alisema Lowassa,ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema .
Alisema uongo mwingine ambao unasambazwa ni kuwa Serikali imezuia watu kumtembelea nyumbani kwake jambo ambalo anaamini ni maneno yanayotungwa.
"Watu wanazuiwa kuja nyumbani kwangu, eti Serikali imezuia hivyo wanakuwa wanaogopa huu ni uongo Serikali haiwezi kuzuia watu kutembeleana," alisema
Irene Uwoya Aondoka na Baraka Zote Kutoka kwa Baba Mzazi wa Marehemu Ndikumana Aagwa kwa Maombi
MSANII wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya ameagwa kwa maombi na baba mzazi wa aliyekuwa mumewe, Hamad Ndikumana,….. na kushukuru kwa baraka hizo jambo lililovuta na kuteka hisia za watu wengi.Katika maombi hayo mafupi, baba mzazi wa marehemu Ndikumana alimtakia safari njema Uwoya ikiwa ni pamoja na baraka tele kwake na mwanaye, Krish ambapo Uwoya aliahidi kushirikiana na familia hiyo kila atakapohitajika kwani tayari ni sehemu yao.
Baba mzazi wa aliyekuwa mumewe, Hamad Ndikumana akimfanyia mambi Irene Uwoya.
“Nenda na baraka zote na hakika nakupa baraka zangu zote wewe na mjukuu wangu Krish na tambua kwamba tunakupenda sana,” alisema baba mkwe wa Uwoya katika maombi hayo mafupi.
“Nawashukuru sana jamani na hakika Mungu awabariki, asante sana Burundi na Mungu awabariki,” alisema Uwoya.
Aliyoyasema kupitia akaunti yake ya Instagram
Asante baba kwa baraka zako …nashukuru mmenipokea vzuri na baraka juuu…MUNGU akubariki sanaaa…tutaonana tena nawapenda sana Mbaki salama…MUNGU ni mwema!!!asante Burundi…
CHADEMA kutoa bima za Afya
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimedai kuwa kitabadilisha fikra
za wananchi pamoja na mazoea ya kwenda hospitali pale wanapokuwa
wanaumwa na badala yake watawajengea uwezo wa kwenda hospitali mara kwa
mara ili kujua Afya zao.
Hayo
yamesemwa na Katibu wa CHADEMA Dar es salam na Mjumbe Baraza kuu na
Mkutano Mkuu Taifa Henry Kilewo ambaye amesema pamoja na kuwajengea
uwezo wananchi watatoa na bima za afya kwa wananchi.
"Chadema
tutakapokuwa Tunaongoza Nchi 2020 tutabadili Fikra za Mazoea Kwa
Wananchi kusubiri Kuumwa ndiyo waende Hospital,Tutawajengea Uwezo wa
Kucheki Afya Zao Mara kwa Mara pamoja na kuwapatia Bima za Afya" Kilewo.
Mbali
na hayo Kilewo amefafanua kwamba ni muda muafaka kwa serikali kuwekeza
kwenye Sekta ya Afya mahali ambapo panadaiwa kuwa na changamoto huku
akikosoa namna Tanzania ilivyo nyuma kwenye sekta ya afya.
Profesa Kitila Mkumbo, Patrobas Kitambi, Albert Msando Wapokelewa Rami CCM
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo ametangazwa rasmi leo
Jumanne mbele ya mkutano wa NEC, CCM unaoendelea Ikulu jijini Dar es
salaam.
Mbali
na Profesa Kitila ambaye alikuwa kada wa ACT, pia kuna Mwenyekiti wa
Bavicha, Patrobas Kitambi , Lawrence Masha, Samson Mwigamba na Albert
Msando.
Akizungumza
mbele ya mkutano huo, Profesa Kitila amesema: "Nguvu ya CCM zipo tano,
moja ni kwamba ni chama cha watu, ni chama pekee chenye nguvu siyo chama
kuogopa watu, tulijaribu huko tulipokuwa lakini yalishindwa."
Kwa
upande wake, Masha amesema alipoamua kuondoka, baba yake alisikitishwa
na uamuzi huo lakini baada ya kutafakari ameamua kurejea nyumbani.
Amesema yeye ni mwanaCCM na kijana alilelewa ndani ya chama hicho.
"Mwenyekiti
wewe ni mfugaji, ng'ombe akiingia zizini amekatwa mkia unamwangalia
mara mbili mbili, mimi sijakatwa mkia ni mwaminifu, ukinihitaji nitumie,
kudumu Chama cha Mapinduzi," amesema Masha.
Kwa
upande wake Mwigamba amesema hoja zote walizopigania Rais John Magufuli
kwa sasa anazitekeleza. Kutokana na hali hiyo analazimika kumuunga
mkono.
"Lakini
ni bahati mbaya wapo wanaoamini upinzani ni kama, tumeamua kuwa moto,
wanaposema huyo amenunuliwa, mie ndiyo naendelea kuwa moto.”
Yeye Msando amesema baada ya kutoka Chadema kwenda ACT amejitambulisha rasmi kujiunga na chama hicho.
Amesema
anafarijika kuona chama hicho na haoni aibu kuwa karibu na CCM tofauti
na ilivyokuwa miaka ya zamani kwani wanachama walihofia kuvaa mavazi ya
chama hadharani kwa kuogopa kuzomewa.
"Kwa sasa chini ya uongozi wako, mtu anajivunia kuwa mwanachama wa CCM, tukaona juhudi zinazoendelea," amesema Msando.
Sophia Simba Aomba Radhi na Kuomba Arejeshwe CCM........Rais Magufuli Akubali Ombi Lake
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Wanawake CCM (UWT), Sophia Simba aomba radhi na kuomba kurejea CCM baada ya kufukuzwa uanachama.
Mwenyekiti
wa CCM Rais John Magufuli amesoma barua ya Sophia kuomba radhi mbele ya
Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na kuwahoji wajumbe kama
wanakubali kumsamehe jambo lililokubaliwa.
"MwanaCCM
aliyefukuzwa uanachama amekuwa akiandika barua nyingi za kuomba radhi
lakini tumekuwa tukinyamaza, kikao hiki ndiyo kilimfukuza," amesema
Rais Magufuli katika kikao hicho kinachofanyika leo Jumanne.
Baada ya kuwahoji wajumbe na kukubaliwa Rais Magufuli aliandika kwenye barua hiyo kuwa amekubaliwa kurudi CCM.
Subscribe to:
Posts (Atom)