Thursday, November 23, 2017

Breaking News: TANZIA: Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama(CCM) afariki dunia


Mchambuzi Huru imepata uthibitisho wa taarifa za kifo cha Mhe. Gama ambacho kinadaiwa kutokea muda wa Saa 6 kuelekea Saa 7 usiku wa kuamkia leo.

Amefariki akiwa mbunge wa Songea Mjini na amefariki dunia usiku wa kuamkia leo hii Songea katika Hospitali ya Peramiho.

Gama amewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Muheza, Nachingwea, Newala, Mbeya na Ilala. Vilevile amewahi kuwa mkuu wa mkoa Kilimanjaro.

Inadaiwa marehemu Gama alianguka nyumbani kwake saa saba usiku juzi huko Likuyu; akapooza upande wa kushoto akawa hajitambui kabisa na akapelekwa Hospitali ya Peramiho ambako aliwekewa mashine za kumsaidia kupumua.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali pema peponi

No comments:

Post a Comment