MASHINJI ATOA NENO KWA ALIYEKUWA KIONGOZI WA BAVICHA KATAMBI AMBAE SASA AMEHAMIA CCM
Katibu Mkuu wa
Chadema, Dk Vincent Mashinji amesema chama hakina mgogoro na aliyekuwa
Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi ambaye ametangaza kujiunga na
CCM kwa kuwa ni haki ya Kikatiba.
Akizungumza na
Mwananchi Jana Jumanne baada ya Katambi kuhamia CCM, Dk Mashinji, “sisi
kama chama msimamo wetu tuliuweka tangu madiwani walivyoanza kuondoka,
tukaweka msimamo wazi kwamba, suala la mtu kuondoka kwenye chama au
kubaki ni suala la Katiba ya nchi ambayo inampa mtu uhuru wa kuhama na
kwenda kwenye chama anachotakana.”
Amesema kuwa haoni sababu ya kumzuia mtu kuondoka kwa kuwa mtu anapoamua kwenda sehemu yoyote anakuwa na matarajio.
Pia, Dk Mashinji
amesema anamtakia heri (Katambi) na kuwataka CCM kumtumia katika sehemu
ambavyo wanaona anafaa kutumika kwa faida ya Watanzania wote.
“Hatuna mgogoro
wowote na kimsingi mimi nimtakie tu heri (Katambi) na wakipenda (CCM)
wamtumie kwenye eneo watakaloona anafaa kutumika kwa faida ya Watanzania
wote,” amesema
Hata Hivyo, Dk Mashinji amesema kuwa walikuwa wanamuandaa Katambi asaidie chama hicho kwenye kitengo cha sheria.
“Alikuwa
anamalizia masomo yake ili awe wakili na tulikuwa tumeshaanza kumuandaa
ili atusaidie kwenye kitengo cha sheria ndani ya chama,”
Katambi ametangaza
leo kujiunga na CCM mbele ya Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC)
unaofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment