Profesa Kitila Mkumbo, Patrobas Kitambi, Albert Msando Wapokelewa Rami CCM
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo ametangazwa rasmi leo
Jumanne mbele ya mkutano wa NEC, CCM unaoendelea Ikulu jijini Dar es
salaam.
Mbali
na Profesa Kitila ambaye alikuwa kada wa ACT, pia kuna Mwenyekiti wa
Bavicha, Patrobas Kitambi , Lawrence Masha, Samson Mwigamba na Albert
Msando.
Akizungumza
mbele ya mkutano huo, Profesa Kitila amesema: "Nguvu ya CCM zipo tano,
moja ni kwamba ni chama cha watu, ni chama pekee chenye nguvu siyo chama
kuogopa watu, tulijaribu huko tulipokuwa lakini yalishindwa."
Kwa
upande wake, Masha amesema alipoamua kuondoka, baba yake alisikitishwa
na uamuzi huo lakini baada ya kutafakari ameamua kurejea nyumbani.
Amesema yeye ni mwanaCCM na kijana alilelewa ndani ya chama hicho.
"Mwenyekiti
wewe ni mfugaji, ng'ombe akiingia zizini amekatwa mkia unamwangalia
mara mbili mbili, mimi sijakatwa mkia ni mwaminifu, ukinihitaji nitumie,
kudumu Chama cha Mapinduzi," amesema Masha.
Kwa
upande wake Mwigamba amesema hoja zote walizopigania Rais John Magufuli
kwa sasa anazitekeleza. Kutokana na hali hiyo analazimika kumuunga
mkono.
"Lakini
ni bahati mbaya wapo wanaoamini upinzani ni kama, tumeamua kuwa moto,
wanaposema huyo amenunuliwa, mie ndiyo naendelea kuwa moto.”
Yeye Msando amesema baada ya kutoka Chadema kwenda ACT amejitambulisha rasmi kujiunga na chama hicho.
Amesema
anafarijika kuona chama hicho na haoni aibu kuwa karibu na CCM tofauti
na ilivyokuwa miaka ya zamani kwani wanachama walihofia kuvaa mavazi ya
chama hadharani kwa kuogopa kuzomewa.
"Kwa sasa chini ya uongozi wako, mtu anajivunia kuwa mwanachama wa CCM, tukaona juhudi zinazoendelea," amesema Msando.
No comments:
Post a Comment