WADAU WA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA WAKUTANA KUJADILI MPANGO KAMAMBE WA USAFIRI WA ANGA ( CIVIL AVITIATION MASTER PLAN) JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt Leonard Chamuriho(katikati) Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari(Kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Mhandisi George Sambali (kushoto) wakiwa kwenye warsha ya kujadili rasimu ya Mpango Kamambe Sekta ya Usafiri wa Anga( The Civil Aviation master Plan) warsha hiyo ilifanyika katika ofisi za Makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) ), Banana - Ukonga jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt Leonard Chamuriho akifungua warsha ya kujadili rasimu ya Mpango Kamambe wa Sekta ya Usafiri wa Anga( The Civil Aviation master Plan) iliyofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA). Banana - Ukonga jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wadau mbali mbali wa sekta ya usafiri wa anga wakishiriki warsha ya kujadili rasimu ya Mpango wa Sekta ya Usafiri wa Anga( The Civil Aviation master Plan) uliofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Banana - Ukonga jijini Dar es Salaam leo.
Wadau wa
sekta ya Usafiri wa anga nchini ,wamekutana katika warsha ya siku moja kujadili
rasimu ya mpango kamambe wa usafiri wa anga
yaani ( the Civil Aviation Master Plan) makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini(TCAA),
Banana-Ukonga.
Warsha hiyo iliyowakutanisha wadau kutoka Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, mashirika yanayotoa
huduma za usafiri wa anga nchini ,
Mamlaka ya Viwaja vya Ndege na mwenyeji Mamlaka ya Usafiri wa Anga imefunguliwa rasmi na Katibu Mkuu Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt Leonard Chamuriho.
Lengo la warsha
hiyo ni kupata maoni ya wadau kuhusu rasimu hiyo ya mpango kamambe wa sekta ya
usafiri wa anga nchini ambayo
imetayarishwa na kampuni ya LEAPP ya Australia chini ya udhamini wa Benki ya
Dunia. Kampuni hiyo ilianza kuanda rasimu hiyo mwaka 2015 kazi ambayo
imefanyika kwa miezi 12.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo , katibu Mkuu wa
wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amesema lengo la serikali ni
kuwezesha Tanzania kutoa huduma za
usafiri wa anga kwa mujibu wa viwango na
taratibu zinazokubaliwa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani
(ICAO) pamoja na kuweka mazingira mazuri yatakayoruhusu ushindani wa kibiashara katika sekta hii.
Ameongeza
kuwa sekta ya usafiri wa anga imekuwa ikikua , mathalani takwimu zinaonyesha safari za ndege
zimeongezeka kwa asilimia 8 katika mwaka
2015 ikilinganishwa na zile zilizofanyika mwaka 2014. Kadhalika idadi ya abiria
imekuwa ikikua kwa kiwago cha asilimia 1.5- 2 kwa mwaka.
Lengo la warsha
hiyo ni kupata maoni ya wadau kuhusu rasimu hiyo ya mpango kamambe wa sekta ya
usafiri wa anga nchini ambayo
imetayarishwa na kampuni ya LEAPP ya Australia chini ya udhamini wa Benki ya
Dunia.
BENKI YA KILIMO
YAJIDHATITI KUSAIDIA UPATIKANAJI WA MASOKO NCHINI
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB),
Bw. Thomas Samkyi (Kushoto) akiwa naMkurugenzi wa Biashara na Mikopo Bw.
Robert Pascal wakifuatilia mada wakati wa Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya
Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB), Bw. Robert Pascal (Kulia) akiwasilisha Mada kuhusu
Wajibu wa TADB katika kuendeleza kilimo nchini wakati wa Warsha ya
Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue
Pearl, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo, na Uvuvi, Mhe. William Ole Nasha
(Kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya
Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Wapili kulia)
wakati wa Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika
katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania, Bibi Janet Bitegeko ambaye pia ni
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TADB
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo, na Uvuvi, Mhe. William Ole Nasha (Kulia)
akizungumza na Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Tanzania, Dkt. Sinare
Yusuf Sinare (Kushoto) na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo
ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Wapili Kushoto) wakati wa
Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli
ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Tanzania, Dkt. Sinare Yusuf Sinare
(Wapili kushoto) akizungumza na Balozi wa Norway nchini, Mhe.
Hanne-Marie Kaarstad (Kushoto) wakati wa Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya

Salaam. Wanaomsikiliza ni Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo, na Uvuvi, Mhe.
William Ole Nasha (Kulia), Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo
ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Wapili kulia) na Afisa
Mtendaji Mkuu-SAGCOT, Bw. Geoffrey Kireng
Mbunge wa Babati Vijijini, Mhe. Jitu Soni (Kulia) akizungumza na

Tanzania (TADB), Bw. Robert Pascal (Katikati) wakati wa Warsha ya

Pearl, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mmoja wa wadau waliohudhuria
warsha hiyo.

akiagana na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Katikati) na Mwenyekiti wa Baraza la
Kilimo Tanzania, Dkt. Sinare Yusuf Sinare (Kushoto) mara baada ya
kufungua Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika
katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam.

Bw. Thomas Samkyi (Wapili Kushoto) akizungumza na Mbunge wa Babati
Vijijini, Mhe. Jitu Soni (Kulia) wakati alipotembelea Meza ya TADB

katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni

(Wapili kulia) na Afisa Maendeleo ya Biashara Mwandamizi wa TADB, Bw.
George Nyamrunda.
Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania
(TADB), Bw. Saidi Mkabakuli akitoa maelezo ya kuhusu TADB kwa mmoja wa
wadau waliotembela Meza ya TADB wakati wa Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya

Mbunge wa Babati Vijijini, Mhe. Jitu Soni (Kulia) akioneshwa moja ya
bidhaa zilizokuwa zikioneshwa katika Meza ya TADBwakati wa Warsha ya

Pearl, jijini Dar es Salaam. Anayemuonyesha ni Afisa Maendeleo ya
Biashara Mwandamizi wa TADB, Bw. George Nyamrunda.
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imedhamiria kusaidia
upatikanaji wa Masoko ili kuongeza Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya
Kilimo nchini ili kuchagiza na kusaidia kuwezesha Sekta ya Kilimo kutoka
kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha kibiashara ili kukuza uchumi na
kupunguza umaskini nchini.
Akizungumzia katika Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo
inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam, yenye
Mada Kuu ya Warsha hiyo, “Wazalishaji Tuanze na Soko, Mkurugenzi
Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi amesema kuwa ukosefu wa masoko ya
mazao unaowakabili wakulima umekuwa ni moja ya changamoto kuu
zinazorudisha nyuma maendeleo ya sekta ya kilimo nchini.
Bw. Samkyi amesema kuwa ili kusaidia kutokomeza changamoto hiyo na
nyinginezo Serikali iliamua kuanzisha TADB ili kusaidia kukabiliana na
mapungufu hayo na kuhuisha upatikanaji wa mikopo na masoko katika sekta
ya kilimo ili kuleta mapinduzi katika kilimo nchini.
“Katika kutekeleza majukumu yetu Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania
imeanza huduma zake kwa kulenga minyororo michache ya ongezeko la
thamani katika kilimo ambapo mikopo ya aina mbalimbali hutolewa
kuwezesha wakulima kuongeza tija na uzalishaji katika sekta ya kilimo
nchini Tanzania,” alisema Bw. Samkyi.
Kwa mujibu wa Bw. Samkyi, Benki inatoa mikopo kwa ajili ya uwekezaji
kwenye ujenzi viwanda vya kusindika mazao, ununuzi wa mitambo na
ufungaji wa mitambo ya usindikaji wa mahindi na kuongeza thamani,
ununuzi wa vifaa vya uvunaji wa kisasa wa mahindi, vifungashio vya
kisasa vya kuhifadhia mahindi na teknolojia ya uhifadhi wa mahindi
kupunguza upotevu wa mazao.
“Kwa sasa tumejikita katika mnyororo mzima wa uongezaji wa thamani
kuanzia uandaaji wa shamban hadi kwa upatikanaji wa masoko, ikiwemo
mahitaji ya uzalishaji wenye tija kwenye sekta nzima ya kilimo kuanzia
hatua za awali za utayarishaji wa mashamba, kupima ubora wa udongo na
virutubisho vinavyohitajika kwenye uzalishaji wa mahindi, upatikanaji wa
pembejeo za kilimo zikiwemo mbegu bora, mbolea, madawa na vifaa na
teknolojia mbali mbali za umwagiliaji na fedha kwa ajili ya kulipia
gharama mbalimbali za uzalishaji wa mahindi,” aliongeza.
Mkurugenzi Samkyi, ameongeza kuwa Benki imejipanga kutoa mikopo ya
ununuzo wa mitambo na mashine za ukaushaji, usafishaji na uchambuzi wa
madaraja ya mahindi pamoja na mitambo ya usindikaji na usagaji wa nafaka
na ujenzi wa viwanda vya kusindikia mazao ikiwamo fedha kwa ajili ya
kulipia gharama mbalimbali za uendeshaji katika kuongeza thamani ya
mazao
Pia, Benki inatoa mikopo kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa
miundombinu ya kilimo katika kuimarisha minyororo ya thamani katika
kilimo ambapo inajumuisha ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji na
mitambo ya umwagiliaji, uchimbaji wa visima vya maji ya umwagiliaji,
ujenzi wa mabawa ya uvunaji maji ya mvua, ujenzi wa maghala bora ya
kuhifadhia mahindi na ujenzi wa miundombinu ya masoko.
Akizungumzia aina ya mikopo itolewayo na benki hiyo, Mkurugenzi wa
Biashara na Mikopo Bw. Robert Pascal amesema kuwa Benki inatoa mikopo ya
aina tatu ambayo ni Mikopo ya muda mfupi (Short term loans), mikopo hii
ni ya muda mfupi usiozidi miaka miwili (au miezi 24), Mikopo ya muda wa
kati (Medium term loan), mikopo ya muda wa kati hutolewa kwa kipindi
cha miaka 2 hadi 5 (yaani kati ya miezi 24 na 60) na Mikopo ya muda
mrefu, mikopo hii hutolewa kwa ajili ya kugharamia shughuli za uwekezaji
mkubwa kwenye kilimo na ambazo marejesho yake yatafanyika katika
kipindi cha miezi 60 hadi 180 (yaani kati ya miaka 5 hadi 15).
Bw. Pascal ameongeza kuwa riba itozwayo kwa upande wa Mikopo ya muda
mfupi (Short term loans) ni riba ya asilimia saba (7%) mpaka (8%) kwa
mwaka. Ambapo mikopo hii Hutolewa kwa ajili ya kufanikisha shughuli za
kilimo kwenye mnyororo wa thamani. Kwa mfano, kugharamia shughuli za
kilimo zinazofanywa kabla ya mazao kuvunwa, na mara baada ya kuvunwa,
ununuzi wa mazao, ununuzi wa zana na mashine za kilimo na mahitaji
mengine ya kifedha katika mnyororo wa thamani.
Ameongeza kuwa mikopo ya muda wa kati hutolewa kwa kipindi cha miaka 2
hadi 5 (yaani kati ya miezi 24 na 60) na hutozwa riba ya asilimia tisa
(9%) mpaka (10%) kwa mwaka. Na mikopo hii hutolewa ili kufanikisha
mahitaji maalumu, mathalani: kupanua mashamba, kuzalisha aina
mpya za mbegu, mifugo, na samaki na kuongeza kiwango cha rasilimali au
uwekezaji, kuboresha miundombinu, pamoja na kuziba pengo la mahitaji
mengine ya muda wa kati kwenye mnyororo wa thamani.
Na kwa upande wa Mikopo ya muda mrefu hutozwa riba ya asilimia kumi na
moja (11%) mpaka (12%). Mikopo hii hutolewa kugharamia mahitaji ya muda
mrefu, mathalani: gharama za kupata rasilimali, kujenga miundombinu
mikubwa ya kilimo, kupanua mashamba makubwa na ya kati, pamoja na
shughuli nyingine za kilimo zinazohitaji mikopo ya muda mrefu. Mikopo
ya muda mrefu inalenga kufanikisha uwekezaji kwenye miradi ya kilimo,
ufugaji, uvuvi na mahitaji mengine ya muda mrefu.
“Mikopo hii hutolewa kwa ajili ya kujenga/kukarabati miundombinu katika
sekta ya kilimo kwenye mnyororo wa thamani, kwa mfano: skimu/mifumo ya
umwagiliaji, maghala ya kisasa ya kuhifadhia mazao, pamoja na mahitaji
mengine ya miundombinu ya kilimo,” aliongeza Bw. Pascal.
TADB ilianzishwa kwa Sheria Namba 5 ya mwaka 2006 inayosimamia Benki na
Taasisi za Fedha, pamoja na Kanuni za Uanzishaji wa Benki na Taasisi za
Fedha (Development Finance) za mwaka 2012. Lengo la msingi la kuanzishwa
kwa TADB ni kutoa mikopo ya muda mfupi, kati na muda mrefu kwa sekta ya
kilimo ili kuleta mapinduzi ya kilimo nchini.
Habari na picha na:
Bw. Saidi Mkabakuli

(TADB)
Copy the BEST Traders and Make Money : http://ow.ly/KNICZ

No comments:
Post a Comment