Wednesday, March 30, 2016



140616Messi-jpg
Kwenye mchezo wa soka kwa sasa kuna vita kubwa kati ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo. Vita hiyo imepelekea mpaka baadhi ya mashabiki kupoteza uhai.Messi amefanikiwa kuitumikia timu ya taifa ya Argentina kwa kucheza mechi 107 mpaka sasa na amefanikiwa kufunga magoli 50, akiwa nyuma ya mchezaji wa zamani wa timu hiyo Gabriel Batistuta ambaye alicheza mechi 78 na kufunga magoli 56.

Miaka kadhaa iliyopita kabla ya kupewa kitambaa cha unahodha, Messi alionekana hafanyi vizuri kwenye timu ya taifa wakati kwenye timu yake ya Barcelona alikuwa anaonekana kuwa mwiba mkali na kuchukua tuzo kadhaa za mchezaji bora.
‘Hakuna marefu yasiyo na ncha’, kilikuwa ni kipindi cha mpito kwa Messi, baada ya kitambaa cha unahodha kupita kwa Javier Mascherano na Carlos Tevez hatimaye kikamuangukia Messi.

Hakuna anayependa kufungwa kwenye mchezo wa soka, baada ya muda lawama zote za kufanya vibaya kwa Messi zimefutika na mashabiki wengine wameenda mbali zaidi kwa kumfananisha na Maradona aliyeichezea timu hiyo ya taifa kwa miaka 17, akicheza mechi 91 na kufunga magoli 34.

Maajabu ya Messi yalionekana kuwakuna mashabiki wengi kwenye fainali za kombe la dunia 2014 zilizofanyika nchini Brazil, timu ya Argentina ilipambana na New Zealand kwenye hatua ya robo fainali. Hakika Messi alionyesha ubora wake wa kustahili kuvaa kitambaa cha unahodha.

Gabriel Batistuta anaongoza kuwa mfungaji wa muda wote kwenye timu ya taifa ya Argentina, amefanikiwa kufunga magoli 56, Messi 50, Hernan Crespo 35, Diego Maradona 34 na Sergio Aguero 32.
Messi ni mchezaji aliyeweka rekodi ya dunia kwa kuchukua tuzo ya mchezaji bora kwa mara tano huku mpinzani wake Ronaldo akifanikiwa kuchukua mara tatu.

No comments:

Post a Comment