Wanajeshi wa Syria wakiwa na bendera ya nchi hiyo baada ya kuukombowa tena mji wa Palmyra. (27.03.2016)
Vikosi ya
serikali ya Syria vikisaidiwa na mashambulizi ya anga ya Urusi Jumapili
(27.03.2016) vimeukombowa tena mji wa kale wa Palmyra uliokuwa
ukishikiliwa ma kundi la Dola la Kiislamu tokea mwezi wa Mei.
Vyombo
vya habari vya taifa na shirika la uangalizi wa haki za binaamu vimesema
mji huo wa kale wa miaka 2,000 ambao ni turathi ya Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uko kwenye mikono ya
serikali baada ya mapigano makali yaliyodumu kwa wiki kadhaa.
Duru za
kijeshi zimeliambia shirika la habari la Ufaransa (AFP) kwamba "baada ya
mapigano makali ya usiku jeshi lina udhibiti kikamilifu mji wa Palmyra
ikiwa ni mji wenyewe wa kale na vitongoji vya wakaazi wa mji huo."
Shirika
la Uangalizi wa Haki za Binaadamu la Syria limesema milio ya risasi
ilikuwa bado ikiendelea kusikika Jumapili katika eneo la mashariki ya
mji huo lakini wapiganaji wengi wa kundi la Dola la Kiislamu walikuwa
wameondoka kutoka mji huo.(P.T)
Watu 300 walijeruhiwa kwenye shambulio hilo
Kundi
moja lililojitenga kutoka kwa wapiganaji wa Taliban limesema ndilo
lililotekeleza shambulio la kujitoa mhanga mjini Lahore, Pakistan
lililoua watu zaidi ya 70.
Kundi
hilo la Jamaat-ul-Ahrar lilisema liliwalenga Wakristo waliokuwa
wakisherehekea Pasaka, ingawa polisi wamesema bado wanachunguza madai
hayo.
Kulikuwa na hali ya kutamausha wazazi wakiwatafuta watoto wao kwenye vifusi.
Rais wa Pakistan ameshutumu shambulio hilo na serikali ya jimbo imetangaza siku tatu za maombolezo.
Takriban watu 300 walijeruhiwa, na maafisa wanasema idadi ya waliofariki inatarajiwa kuongezeka.
Mlipuko huo ulitokea kwenye bustani ya Gulshan-e-Iqbal mjini Lahore karibu na eneo la kuchezea watoto Jumapili jioni.
Shambulio lilitokea karibu na eneo la kuchezea watoto
Lahore ni mji tajiri na ni mojawapo wa miji yenye mtazamo huru zaidi nchini Pakistan.
Ndiyo
ngome ya kisiasa ya waziri mkuu wa sasa Nawaz Sharif, na haujakuwa
ukishuhudia mashambulio mengi ya kigaidi miaka ya karibuni.
Msemaji
wa kundi la Jamaat-ul-Ahrar, Ehsanullah Ehsan, alisema kundi hilo
lilitaka kutuma ujumbe kwa Bw Sharif kwamba wameingia Lahore na akasema
kundi hilo litatekeleza mashambulio zaidi.
Jamaat-ul-Ahrar
walijitenga kutoka kwa Tehrik-e Taliban Pakistan. Limetekeleza
mashambulio mengine kadha dhidi ya raia na vikosi vya usalama miezi ya
hivi majuzi.
Bw Sharif ameeleza masikitiko yake na huzuni kutokana na watu wengi wasio na hatia waliopoteza maisha yao.
Ameahirisha ziara aliyokuwa amepanga kuifanya nchini Uingereza.BBC
No comments:
Post a Comment