CHAD YAJITOA AFCON 2017
Timu ya Taifa ya Chad ‘Les Sao’
imejiondoa katika michuano ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa
Afrika (AFCON) itakayofanyika mwaka 2017 nchini Gabon.
Taarifa ya kujitoa kwa Chad
imetolewa na Shirikisho la Mpira wa miguu barani Afrika (CAF) leo baada
ya Les Sao kuandika barua ya kujitoka katika mashindano hayo ikiwa
katika kundi G pamoja na timu za Tanzania, Nigeria na Misri.
Chad ilitarajiwa kucheza kesho
Jumatatu dhidi ya Tanzania katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,
ikiwa ni mchezo wa marudiano wa kundi G baada ya kucheza mchezo wa awali
jijini N’Djamena katika ya wiki.
Katika mchezo wa awali uliochezwa
uwanja wa Idriss Mahamat Ouya, Taifa Stars iliibuka na ushindi wa bao
1- 0 , bao lililofungwa na nahodha Mbwana Samatta dakika ya 30 ya
mchezo.
Kufuatia kujitoa kwa Chad,
matokeo ya michezo yote iliyoihusisha timu hiyo yanafutwa, na msimamo wa
kundi G kwa sasa unaongozwa na Misri yenye pointi 4, Nigeria pointi 2
na Tanzania pointi 1.
TAMASHA LA PASAKA LAPAGAWISHA MASHABIKI WA MUZIKI WA INJILI CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizindua rasmi albam mpya ya mwimbaji
Goodluck wakati wa tamasha la Pasaka lililofanyika kwenye uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza leo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa
wa Mwanza , Wabunge pamoja na Maaskofu wa makanisa ya Mwanza.
Tamasha hilo ambalo limehudhuriwa
na mashabiki wengi mkoani humo limetumbuizwa na waimbaji mbalimbali wa
nyimbo za injili kutoka hapa nchini na nchi jirani za Zambia na Kenya,
waimbaji hao ni Upendo Nkone , Martha baraka , Jesca BM, Joshua Mlelwa ,
Tumsifu Rufutu, Christopher Mwahangila, Jeniffer Mgendi, Bonny
Mwaiteje, Goodluck ambaye amezindua albam yake mpya na waimbaji Faustine
Munishi kutoka nchini Kenya, Solomon Mukubwa kutoka Nchini Kenya pamoja
na Ephraim Sekereti kutoka nchini Zambia wote kwa pamoja wamefanya
maonesha mazuri yaliyopagawisha mashabiki wa muziki wa injili katika
uwanja wa CCM Kirumba na kuwafanya wacheze kila wakati, katika picha
kulia ni mwimbaji Goodluck na kushoto ni Bw. Alex Msama Mkurugenzi wa
kampuni ya Msama Promotion inayoandaa matamasha hayo.
Tamasha hilo litaendelea kesho
kwa onesho kabambe linalotarajiwa kufanyika mjini Kahama mkoani
Shinyanga baada ya kumaliza maonyesho mawili katika mikoa ya Geita na
Mwanza.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-MWANZA)
Waziri wa Habari,
Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye wa nne kutoka kulia
akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. John Mongela alipokuwa
akimkaribisha rasmi ili kutoa salam zake kutoka kwa serikali.
Waziri wa Habari,
Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akishiriki katika sala maalum
ya kuombea albam ya mwimbaji Goodluck wa pili kutoka kulia iliyotolewa
na maaskofu wa mwanza kabla ya kuizindua
Waziri wa Habari,
Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akishuka kutoka jukwaani kwa
ajili ya kuizindua rasmi albam hiyo na kutoa salaam za serikali katika
tamasha la Pasaka.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. John
Mongela akipokewa na Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mh. Baraka Konisaga
kushoto na Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama wakati
alipowasili kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mh.
Baraka Konisaga akipokewa na Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex
Msama wakati alipowasili kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndugu Miraji Mtaturu akiinunua albam ya mwimbaji Goodluck mara baada ya kuzinduliwa rasmi na Waziri
wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye kwenye tamasha la
Pasaka lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Waziri wa Habari,
Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akitoa salam zake na kukemea
watu wanaojihusisha na wizi wa kazi za wasanii na kusema serikali ya
awamu ya tano itahakikisha wahusika wote wanashughulikiwa vya kutosha
ili kuhakikisha wasanii wanapata haki yao katika kazi zao na jasho lao.
Mwimbaji Goodluck akiimba mara
baada ya kuizindua rasmi albam yake kwenye tamasha la pasaka jijini
Mwanza lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Mwimbaji Upendo Nkone akifanya vitu vyake jukwaani na kuwarusha vya kutosha mashabiki waliohudhuria katika tamasha hilo.
Waziri wa Habari,
Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akiongoza na viongozi
mbalimbali pamoja na baadhi ya maaskofu kucheza wakati mwimbaji Upendo
Nkone alipokuwa akiimba jukwaani.
Waziri wa Habari,
Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akipiga picha ya pamoja na
waimbaji wa muziki wa injili mara baada ya tamasha hilo kumalizika
kutoka kulia ni Bonny Mwaiteje. Jesca BM na Upendo Nkone.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akicheza wakati mwimbaji Bonny Mwaiteje alipokuwa akitumbuiza.
Mwimbaji Bonny Mwaiteje akifanya vitu vyake jukwaani
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mh.
Baraka Konisaga akipunga mkono huku akicheza na baadhi ya viongozi wa
mkoa wa Mwanza na maaskofu pamoja na wachungaji wakati mwimbaji Upendo
Nkone akifanya vitu vyake jukwaani.
Roho wa Bwana Yesu akiwashukia
mashabiki wa muziki wa injili wakiwa wamenyanyua mikono yao juu juu
wakati mwimbaji Upendo Nkone alipokuwa akiimba jukwaani.
Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion pamoja na Mkewe wakielekeakuketi jukwaa kuu.
Waziri wa Habari,
Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akipokelewa na Alex Msama na
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. John Mongela alipowasili uwanja wa CCM
Kirumba.
Mwimbaji Martha Baraka akitumbuiza katika tamasha hilo.
Naye Mwimbaji Jeniffer Mgendi akafanya mambo makubwa jukwaani kama anavyoonekana.
Bw. Alex Msama kulia akiwa na Mkewe katikati pamoja na MC wa matamasha ya Pasaka MC Mwakipesile.
Mmoja wa washabiki ambaye ni mlemavu alishindwa kujizuia akaamua kucheza kama anavyoonekana katika picha.
Mwimbaji Joshua Mlelwa amefanya mambo makubwa jukwaani katika tamasha hilo kama kawaida yake.
Mashabiki wakicheza kwa furaha katika tamasha hilo.
Mwimbaji Faustine Munishi kutoka nchini Kenya akipagawisha mashabiki na nyimbo zake za kuabudu kama vile “Malebo”.
Mwimbaji Christopher Mwahangila akiwapa upako mashabiki kupitia injili ya uimbaji.
Mwimbaji Ephraimu Sekereti kutoka nchini Zambia naye akaimba nyimbo za kusifu na kuabudu.
Solomon Mukubwa akiafunga kazi na nyi,bo zake kali zilizowafanya mashabiki kuwa wima wakati wote kama wanavyoonekana.
No comments:
Post a Comment