Baada ya Kuachwa na Mbunge na Kulazwa..Yasemekana Wastara Juma Atoroshwa Hospitalini
Taarifa
mbaya! Staa wa Bongo Muvi, Wastara Juma ambaye mapema wiki iliyopita
alidai kupewa talaka la mumewe, Sadifa Khamis Juma, Mbunge wa Donge,
Zanzibar, anadaiwa kutoroshwa hospitalini kisha kupelekwa hoteli ya
mafichoni huku akiendelea na matibabu.
Kwa
mujibu wa chanzo makini, Wastara aliyekuwa amelazwa kwenye Hospitali ya
Misheni ya St. Herry Health Center iliyopo mjini hapa, aliondolewa
wodini hapa usiku mnene huku akiwa bado hali yake ya kiafya
haijatengamaa tangu alipolazwa mapema wiki iliyopita akisumbuliwa na
presha na kisukari na baadaye kupoteza fahamu.
Wikienda
lilifika hospitalini hapo Jumamosi iliyopita na kuthibitishiwa
kuondolewa kwa msanii huyo na mtu aliyedai kuwa ni babu yake aliyetajwa
kwa jina la Abdulaziz Babu.
Kwa
mujibu wa mmoja wa wahudumu waliokuwa zamu walioomba hifadhi ya majina,
jamaa huyo alidai kuwa Wastara aruhusiwe kwani alihofia usalama wake na
kwamba sehemu aliyopanga kumpeleka ni salama zaidi.
Baada
ya kunusa ‘ubuyu’ huo hospitalini hapo, Wikienda lilimsaka Wastara
kujua mahali alipo na hali yake lakini jitihada hizo ziligonga mwamba
kwa kuwa namba yake ya simu haikuwa hewani.
Alipotafutwa mtu huyo anayedai ni babu wa Wastara alifunguka: “Ni
kweli nimemuondoa Wastara hapo hospitalini kwa sababu za kiusalama.
Yupo hotelini lakini siwezi kukuelekeza ni sehemu gani kwa sababu
ukiandika itajulikana na tatizo litakuwa palepale.”
Wastara
alikumbwa na hali hiyo ikidaiwa ilitokana na mgogoro wa ndoa yake na
Sadifa iliyofungwa hivi karibuni na kushindwa kudumu.
Bonyeza HAPA kudownload application ya Udaku Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Kwa Urais
No comments:
Post a Comment