Miaka 5 jela kumkosoa rais wa Angola
- Dakika 27 zilizopita
Mwanamuziki wa
kufoka kutoka Angola amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa tuhuma za
uhaiani na njama za kumpindua rais dos Santos.
Luaty Beirao anatuhumiwa kwa kupanga njama ya kumpindua rais Jose Eduardo dos Santos.Mwanamuziki huyo mashuhuri alifikishwa mahakamani mjini Luanda pamoja na washirika wake wengine 16 na wakahukumiwa vifungo vya kati ya miaka 2 hadi 8.
Wanaharakati hao 17 walikamatwa mwezi Juni walipopatikana wakijadili kitabu kimoja kilichokuwa na mada ya kutafuta mbinu isiyo ya kutumia nguvu kuleta mabadiliko nchini.
Rais dos Santos ametawala Angola tangu mwaka wa 1979.
Beirao, ambaye anatumia jina la usanii la ''Ikonoklasta'', amekuwa mkakamavu kuikosoa serikali, na kutaka ugavi sawa wa raslimali miongoni mwa maskini waliowengi nchini humo.
Mwezi septemba mwaka uliopita alisusia kula na kunywa katika jitihada za kuishinikiza serikali kumuachilia hru.
Jaji alitoa hukumu hiyo kufuatia mashtaka ya kupanga njama dhidi ya rais wa jamhuri kughushi stakabadhi rasmi za serikali na kujiunga na kundi haramu.
Maelfu ya watu wamekasirishwa na hukumu hiyo wakidai ni hujuma dhidi ya wale wanaomkosoa rasi Dos Santos.
No comments:
Post a Comment