Mtoto afariki dunia kwa kutumbukizwa
katika kisima cha maji na baba yake
mzazi Morogoro.
Katika hali isiyo ya kawaida mtoto mmoja aliye julikana
kwa majina ya Elena Mussa mwenye umri wa mwaka
mmoja na miezi mitano mkazi wa kijiji cha Mazoka
wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro amekutwa
akiwaamekufa ndani ya kisima cha maji kwa kile
kilicho daiwa kudumbukizwa na baba yake mzazi
mwenye matatizo ya akili kwa muda mrefu.
Wakizungumza na ITV mashuhuda wa tukio hilo na
ndugu wa marehemu wamesema wakati walipo enda
kuchota maji katika kisima hicho waliuona mwili wa
mtoto huyo ukielea majini kisha kutoa tarifa kwa
mwenyekiti wa kijiji.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha Rozi
amesema baada ya kuona tukio hilo alitoa tarifa Polisi
ndipo taratibu za kutoa mwili huo zilianza huku babu
wa marehemu Bwana.Mwanangumi Makala akieleza
jinsi kifo cha mjukuu wake kilivyo tokea.
Kwaupande wake mganga wa Hospital ya wilaya ya
Kilosa Julius Chiduo amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo ambapo akitoa taarifa za uchunguzi wa mwili wa
marehemu amesema mtoto huyo amefariki baada ya
kukosa hewa kwa kuzibwa pua na kushindwa kupumua
jambo ambalo limepelekea kupoteza uhai wake.
No comments:
Post a Comment