Hiki ndiyo kiashiria cha AY kufanya tour na Diamond Platinumz
0
Muziki
wa Tanzania unazidi kukua zaidi na kuwa moja ya nchi ambayo inatazamwa
zaidi katika soko la muziki kwa bara la Afrika ambapo msanii Diamond
Platinumz amekuwa mbele akiongoza katika orodha ya wasanii ambao
wanapeperusha bendera ya Tanzania kimataifa.
Aidha
Diamond kwa sasa anafanya ziara barani Ulaya katika nchi mbalimbali
ambapo kupitia akaunti zake za mitandao mbalimbali ya kijamii amekuwa
akionyesha jinsi shoo zake zinafanyika vizuri kwa kuwaburudisha
mashabiki wake katika nchi hizo.
Moja ya video ambayo video aliweka Instagram alionekana akiimba wimbo wa Zigo Remix ambao alishirikishwa na AY na kuandika “About last Night in STOCKHOLM SWEDEN… @aytanzania you need to watch this #ZigoRemix …..add me on Snapchat…. Dplatnumz Dplatnumz#FromTandaleToTheWorldTour”
Baada ya kuweka video hiyo AY ali’repost’ na kuongeza maneno “I SEE U MAN ENDELEA KUWAKILISHA,SOON TUTAZUNGUKA PAMOJA” ambapo
kwa namna moja au nyingine maneno hayo ni kiashiria tosha kuwa AY
anataraji kufanya ziara za kimuziki akiwa na staa mwenzake Diamond.
Kama
wadau wa muziki nchini tusubiri kuona ni jambo gani litafuata baada ya
maneno hayo ya matumaini kwa Watanzania kuona muziki wao ukikua zaidi.
No comments:
Post a Comment