Urais 2015: Chama cha ACT – Wazalendo kutoa fursa kwa watangaza nia
Chama cha ACT-Wazalendo kintarajia kutoa fursa kwa watangaza nia wa
nafasi mbalimbali katika mkutano wake wa kitaifa utakaofanyika tarehe 13
mwezi huu.
Hatua hiyo inafuatia joto la urais kuanza kupanda ndani ya
vyama mbalimbali vya kisiasa nchini kikiwemo chama tawala cha Mapinduzi
(CCM).
Kwa mujibu wa Katibu Mawasiliano na Uenezi wa Chama wa ACT –wazalendo
Sabini Richard amesema chama hicho kimejipanga kushiriki katika
uchaguzi mkuu hivyo kutakuwa na mkutano mkuu utakaofanyika mkoani
Tabora.
Katika mkutano huo watahuisha azimio la Arusha lengo likiwa ni
kudumisha misingi ya amani, udugu na uzalendo kwa lengo la kuwaunganisha
watanzania pamoja na kuenzi harakati za ukombozi barani Afrika.
Katika hatua nyingine, Richard amesema katika mkutano huo hicho
wanatarajia kusimamisha wagombea katika nafasi ya Urais na Wabunge na
madiwani katika majimbo yote nchini.
mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment