Shilole kumzalia Nuh Mziwanda?
Mpekuzi blog
Msanii wa muziki nchini Tanzania Nuh Mziwanda, baada ya kuvuka kiunzi
cha skendo ya kumpachika mimba binti na kumkana hadharani, jambo ambapo
lilipelekea msukosuko katika penzi lake na mpenzi wake Shilole,
hatimaye atamka hadharani mipango yake ya kuazaa na Shilole.
Akihojiwa na eNews ya EATV Mziwanda amesema kuwa yeye na Shilole, wanapenda sana kupata mtoto
wao, ila anafahamu kuwa hiyo ni mipango ya Mungu na wakati wowote kutoka
sasa ikitokea baraka hiyo watafurahi.
Amedai kuwa Mungu akiwajalia kuwa na mtoto furaha yao itaongezeka kwa
kuwa kila kitu Mungu ndio mpangaji na kusema kuwa bado yupo kwenye
mipango ya ndoa baada ya kutambulishana kwa wazazi.
No comments:
Post a Comment