Saturday, June 6, 2015

Hiki ndio kilichonifikia kuhusu Makongoro Nyerere kuhusishwa na ajali iliyotokea leo Kigoma

20150606040816Headlines kwenye Magazeti leo nyingi zina stori kuhusu Wagombea wa Urais kwa makada wa CCM wameingia kwenye hatua nyingine ya kupita mikoani kwa ajili ya kutafuta wadhamini wao, Makongoro Nyerere ni mmoja wa Wagombea hao ambae stori zilizoenea mitandaoni leo zinahusu msafara wake uliokuwa Kigoma kupata ajali.
 Stori imekuwa kubwa na wengine wameipata taarifa hiyo tofauti na jinsi ajali iliyotokea.. Nimepita MICHUZI BLOG na kuikuta hii stori, gari iliyopata ajali ni gari iliyokuwa imebeba Wasaidizi wa Makongoro Nyerere.. Gari hiyo imepinduka ikiwa kwenye mwendo wa kasi.
Watu walioumia ni wasaidizi hao pamoja na Mwandishi wa Habari mmoja.
20150606040817Kama kuna kingine kitanifikia kuhusu hii ishu nitakusogezea muda wowote mtu wangu.
Pole kwa wote walioumia kwenye ajali hii.

No comments:

Post a Comment