Saturday, June 6, 2015

Kuna watu ambao walimuita Mzee Majuto kwenye show wakamuahidi kumlipa mil.2, baada ya show wahusika hawakumlipa… Mzee Majuto ikabidi amtafute Wema Sepetu ambae alimuunganisha na watu hao.

Mzee Majuto amesema Wema aliwatafuta watu hao na wakamlipa hela hiyo jana.. lakini hii sio mara ya kwanza kwa Mzee Majuto kutapeliwa, kumbe aliwahi kusainishwa mpaka Mkataba kwenda kwenye show Mwanza yeye pamoja na akina JB na Steve Nyerere, mwishowe wakatapeliwa hivyohivyo.

U Heard iko kwenye hii sauti mtu wangu, Mzee Majuto kasimulia ishu nzima ilivyokuwa pamoja na huo utapeli wa Mwanza.

No comments:

Post a Comment