Majibu ya Diamond kwa Jokate kuhusu post yake iliyoleta utata
Mpekuzi blog
Mshindi huyo wa ‘Best Live Act’ kwenye MTV MAMA baada ya kurejea
Tanzania, amejibu shutuma alizozitoa Jojo dhidi yake kuhusu video
aliyoipost, ya mrembo huyo aliyewahi kuwa mpenzi wake akifurahia wimbo
wa ‘Mdogo Mdogo’ na kuandika “Mbona Bado, Mtanyooka Tu”.
Kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm, haya ndio majibu ya Diamond kuhusu video aliyoipost na kile alichokiandika Jokate:
“unajua kwanza nimecheka afu nimeskitishwa kwasababu nimeambiwa,
sijasoma nimeambiwa kuna post ameandika amezungumzia vitu vingi… Yeye
kacheza kama fan wa nyimbo yangu, na mimi nimempost kama fan wangu, ile
caption yangu sijamuandika jina kwanini achukulie vibaya?
"Ukiona mtu
anajishuku ukiona hivyo kuna namna nyuma. Mbona mi napost watu wengi tu,
tena naandika caption zangu za vituko vituko manake mimi nina caption
za vituko, mi ni mswahili nimezaliwa Tandale nimekulia Tandale na
Tandale ndio kumenifanya leo niwe hapa nilipo…
"kwahiyo nina caption zangu
za uswahili kwasababu uswahili ndio umenikuza…siziachi kuziandika mbona
naziandikaga katika caption nyingi nyingi kwanini kwake yeye tu aione
tatizo, kwani kuna ubaya gani mi kuandika mtanyooka tu kama yeye
haimuhusu ina maana labda kuna kitu kinamuhusu.”
Diamond aliendelea:
“Nikaambiwa pia amezungumza kwamba ndio maana wanaogopa kusapoti
wasanii watanzania kwasababu akisapoti wanadhalilishwa, yeye mimi mpaka
nimeenda kuchukua tuzo hii amenisapoti nini?
"Alipost hata post moja
kusema mpigie kura Diamond, afu leo anajishaua eti kanisapoti, kasapoti
nini eti kutoa hongera mi nimeshinda tuzo, eti ooh hongera kwa tuzo by
the way, angepost kuhamasisha watu wapige kura ili ushindi uje nyumbani,
lakini kwa chuki alizojazwa zisizo na sababu na roho mbaya alowekwa na
watu imemfanya ashindwe hata kunipost na kutengeneza chuki za chini
chini kwa kudhani wakiwapigia kura Wanigeria mi ntakosa tuzo…
"Mungu
alivyolaani mi nimeshinda, afu anajifanya anatoa hongera eti wanasapoti
muziki wa kiTanzania, utanisapoti nini, lini umenisapoti, au baada ya
kuona tuzo imekuja ndo unajifanya kutoa hongera, tuacheni unafiki.” Alimaliza diamond.
No comments:
Post a Comment