Thursday, July 16, 2015

MAPOKEZI YA MBUNGE WA CHADEMA MBOZI MAGHARIBI MH DAVID SILINDE YAVUNJA REKODI

Mbunge wa Mbozi Magharibi Mheshimiwa David Silinde akiwahutubia wakazi wa Tunduma waliompokea.

Msafara wa Magari, Bajaji na Bodaboda uliompokea Mheshimiwa David Silinde.

Wakazi wa Tunduma wakimsikiliza Mheshimiwa David Silinde baada ya kupata mapokezi makubwa.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU CUF NA UKAWA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

15 Julai 2015


CUF NA UKAWA


Waheshimiwa waandishi wa Habari

Chama cha wananchi CUF tukiwa sehemu ya UKAWA tunaendelea na vikao vya kuafikiana na maamuzi kwa hoja mbalimbali zinazohusu uimarishaji wa malengo ya uanzishwaji wa UKAWA.
Katika kikao cha UKAWA kilichofanyika tarehe 14 Julai 2015 Collesium Hotel Dar es Salaam, CUF hatukuweza kushiriki kikao hicho.

Sababu za kutoshiriki kwetu katika kikao hicho, kumetokana na sababu za kikatiba za ndani ya CUF kwa kuwa katika maamuzi yote yanayohusu masuala mazito ya kinchi kama haya,tuna desturi ya kukaa na kujadiliana kama chama kwanza katika kuafikiana na jambo lolote lile muhimu kwa maslahi ya taifa kama vyama vingine vinavyofanya.

Baada ya kikao cha UKAWA cha 11/07/2015 CUF tume kuwa na vikao vinavyohusisha viongozi wakuu wa chama yaani Mwenyekiti,Naibu Katibu Mkuu na wakurugenzi na jana tumeendelea na kikao.

Na ndio maana katika kikao cha UKAWA Mwenyekiti Prof.Lipumba na sisi viongozi wa kuu hatukuweza kuhudhuria.

Kutohudhuria kwa kikao cha tarehe 14 Julai 2015, hakuna mahusiano yoyote na uvumi kwamba CUF imesusia au kujitoa katika UKAWA kama baadhi ya mitandao ya kijamii au vyombo vya habari vilivyoripoti pamoja na maneno ya chini kwa chini yanayoendelea kwa wananchi, bali ni kutokana na baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la taifa kutoka mikoani na wanachama wetu maeneo mengi ya nchi kuutaka uongozi wa Chama kusitisha kwa muda kuhitimisha maamuzi ya kumpata mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupeperusha bendera ya UKAWA mpaka kuwepo kwa ridhaa ya Chombo hicho cha kikatiba.

Aidha Chama kinatambua kwamba hivi sasa tumebakiwa na muda mfupi kabla ya kuingia katika mchakato rasmi wa kuchukua fomu za serikali kuomba kuteuliwa kuwania uongozi, hivyo Chama kimeitisha kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la taifa hapo tarehe 25 Julai 2015 ilikupata Baraka ya chombo cha maamuzi kama ambavyo wenzetu washirika wa UKAWA wamekwishapitia hatua hizi katika vyama vyao.

Watanzania watambue kwamba Nchi inapitia katika kipindi kigumu sana, ongezeko la majimbo 26 ya Uchaguzi yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi,kwa kipindi cha chini ya siku 45 kabla ya kuanza kampeni ni changamoto ambazo UKAWA tunapaswa kuyafanyia kazi ili kuona namna gani tunajipanga kwa mazingira haya.

CUF tuanaamini kwamba kwa maridhiano ya pamoja ndani ya vyama vyetu na ndani ya UKAWA tutajenga UKAWA imara na hatimaye kuwa na mgombea mmoja wa Urais,Wabungena madiwani wa UKAWA na hivyo kuiangusha CCM kwenye uchaguzi wa Oktoba 25.

HAKI SAWA KWA WOTE
Magdalena Sakaya
Naibu Katibu Mkuu, Bara.

CUF: Hatujajiengua UKAWA

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimekanusha uvumi kuwa kimejiengua na kukisusia kikao kinachoendelea cha Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), kwa kile kinachodaiwa kina uchu wa madaraka.

Aidha, CUF imekanusha uvumi kuwa baadhi ya wananchama na wenyeviti wa CUF kununuliwa na Chama cha Mapinduzi ( CCM), kwa lengo la kuuvuruga umoja wao na kuisambalatisha UKAWA.


Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu Bara, Magdalena Sakaya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambamo kimechukua fursa hiyo kuwaonya waandishi kuandika habari za kweli zinazohusu UKAWA kuliko kuandika habari zinazoweza kupotosha umma.

Sakaya ameendelea kusisitiza kuwa, CUF haijajiengua na UKAWA, ambamo amebainisha sababu za kutoshiriki katika kikao cha jana Julai 14,2015 kilichofanyika katika ukumbi wa Collesium Dar, kumetokana na sababu za kikatiba za ndani ya Chama ambapo jana walikaa kikao hivyo kupelekea kushindwa kutuma mwakilishi katika kikao hicho.

“Baada ya kikao cha UKAWA cha Julai 11 mwaka huu CUF tumekuwa na vikao vinavyohusu viongozi wakuu wa Chama akiwemo Mwenye kiti, manaibu katibu wakuu na wakurugenzi na jana ndo tulikuwa na kikao na ndio maana hatukuweza kutoka” amesema Sakaya.

“Kutohudhura katika kikao cha jana hakuna mahusiano yoyote na uvumi na maneno ya chini chini kwa baadhi ya mitandao ya kijamii yanayopotosha umma”

Kuhusu uvumi unaodai kuwa UKAWA umeshampitisha mgombea kwa kupiga kura na kwamba baadhi ya magazeti kumuandika mgombea amesema halina ukweli, taarifa hizo pia zilipelekea baadhi ya wananchama wa CUF kukusanyika makao makuu ya CUF ili kupata ufafanuzi zaidi juu ya uvumi huo.

Nae Mkurugenzi mipango na uchaguzi Shaweji Mketo amesema, kuhusu maneno yanadai kuwa UKAWA ni pasua kichwa na kwamba unakaribia kuvunjika hayana ukweli isipokuwa wanafuata katiba ya kila chama ndipo wamtoe mwali atakaye peperusha bendele ya UKAWA.

Amesema, “niwatoe wasiwasi wananchi na wapenzi wa UKAWA muondoe hofu tupo imara na tunatarajia baada ya siku tano kumtangaza mgombea wetu, na kikubwa kinachojadiliwa sasa ni ugawaji wa majimbo kutokana na kuongezeka kwa majimbo hivyo ni lazma tuyajadili kwa kina na kujua yupi atachukuwa wapi”

Kuhusu kikao cha Baraza kuu la uongozi wa kitaifa Mketo amesema, “tunatarajia kufanya kikao cha mwisho Julai 25 mwaka huu ili kupata Baraka ya chombo cha maamuzi kama ambavyo wezetu wa washiriki wa UKAWA wamekwisha pitia hatua hizo katika vyama vyao”

Wednesday, July 15, 2015

MGOMBEA WA UKAWA KUTANGAZWA NDANI YA SIKU SABA

Mgombea urais ndani ya UKAWA kuja kutangazwa kwa shamrashamra ni ndani ya siku saba.

Ni baada ya kikao (summit) kukamilisha maridhiano ambapo kilizungumzia jinsi gani ya kuachina majimbo yalibaki na swala la mgombe urais

Akiongea na waandishi wa habari mwenyekiti wa NCCR Mageuzi JAMES MBATIA aliwaeleza wanahabari kuwa taratibu zote zimekamilika ndani ya vyama vinavyounda UKAWA na kilichobaki ni jinsi gani ya kumtangaza mgombea urais ndani ya UKAWA kwa kushirikiana na vyama vyote vinavyounda umoja huo, ndani ya siku saba .

Huku akiwasisitiza watanzania kuwa wavumilivu na kuwataka wajitokeze kujiandikisha katika daftari la kudumula wapiga kura linalotegemewa kuanza punde katika mkoa wa Dar es Salaam huku wakitega maskio yao na kumpokea mgombea urais ambaye atatambulishwa kuipeperusha bendera kupitia UKAWA.

Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyeuliza swali
Je, ni kweli kama ilivyotapaka katika mitandao ya jamii juu ya Lowassa Kujiunga na chama kimojawapo ndani vyama vinavyounga UKAWA?

Akijibu swali hilo kwa kulitolea mifano ya mitandao ya jamii inayotumika na watu fulani kwa maswai yao binafsi na sio kuelimisha jamii, Mh Jamse Mbatia ilizungumzia moja ya account ya twitter iliyofunguliwa kwa jina mtandao mkubwa duniani BBC ikieleza kuwa Lowassa tayari ameshajiunga katika chama cha ACT na kusisitiza habari hizo sio za kweli huku akiwashauri watanzania kupima uzito wa habri na chombo kinachokiwasilisha na kuwataka wananchu wafatilie habari za vyama kupitia mitandao ya vyama.



No comments:

Post a Comment