TARIME: Mwenyekiti CHADEMA mbaroni Akidaiwa kuiba Mlingoti wa bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
MWENYEKITI
wa Chama cha Demkrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Kijiji cha Sokini
mji mdogo wa Sirari wilayani Tarime, Denisoni Makanya (44),
amepandishwa kizimbani mbele ya Hakimu, Gibogo Wenje, akidaiwa kuiba
mlingoti wa bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wenye thamani ya Sh
80,000.
Mwendesha Mashtaka wa Oolisi, George Lutonja, alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo usiku Mei 29, mwaka huu.
Mshitakiwa alikana shitaka na yuko nje kwa dhamana hadi Agosti 4 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
No comments:
Post a Comment