Friday, June 5, 2015

Sakata la Picha za UCHI: BASATA Wamsamehe Shilole


Shilole a.k.a Shishi bybee sasa anaweza kupata usingizi mnono bila mawazo, sababu lile sakata la kusambaa kwa picha zake chafu zilizopigwa wakati akitumbuiza nchini Ubelgiji mwezi uliopita hatimaye limemalizika vizuri.

Sakata hilo  lilifika hadi bungeni ambapo Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia alisema serikali ililiagiza Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA kufanya naye mahojiano ili serikali iweze kuchukua hatua.
 
Muimabaji huyo wa ‘Nakomaa na JIji’ ameelezea furaha yake baada ya kusamehewa na BASATA alipoenda kutoa maelezo.
 
“Leo nimeenda BASATA kwasababu waliniita juzi, kwahiyo nimeenda kusikiliza wito wao, tumeongea nashukuru wamenielewa tumeongea tumeelewana basi hakuna tena kitu ambacho kina tatizo tena hapo kwasababu wale ni wazazi wanatakiwa kumkanya mtu kama mtoto labda” Alisema Shishi bybee
 
“Tumeelezana pale nini kifanyike nini kisifanyike na kila kitu ambacho kinahusiana na tasnia ya sanaa. Nimewaelezea situation ilivyotokea wamenielewa wameniambia pia niwe mwangalifu katika mavazi, of-course ni kweli kitu kama hicho kinaweza kutokea kwahiyo sisi ni binadamu, nimeshukuru sana kwasababu wameweza kunielewa, basi ni hivyo tu nina furaha kwaajili ya hiyo kitu.” Alimaliza Shilole.

No comments:

Post a Comment