Lowassa atua jijini Mwanza kusaka wadhamini...Mamia Ya Wananchi Wampokea Huku Wakimwita Rais...! Rais!!
MAELFU
ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM, na wakazi wengine wa jiji la
Mwanza, leo Ijumaa Juni 5, 2015, walifurika kwa wingi kwenye ofisi za
CCM wilaya ya Nayamagana na ile ya Ilemela, wengine wakitaka kumuona na
kupeana mikono na wengine kwa nia ya kumdhamini Waziri Mkuu wa zamani na
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, alipofika jijini Mwanza kutafuta
wana CCM wa kumdhamini katika safari yake ya Matumaini. (Kuwania urais
wa Tanzania kupitia CCM.)
Madereva
texi, waendesha bodaboda, na hata wafanyakazi na wasafiri kwenye uwanja
wa ndege wa Mwanza, waliacha shughuli zao kwa muda ili walau wamuone
mtangaza nia huyo wa nafasi ya juu kupitia CCM.
Lowassa
alichukua fomu, za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania,
Alhamisi Juni 4, 2015 pale makao makuu ya CCM, na safari yake ya kusaka
wadhamini ilianza “chap chap” pale pale Dodoma, na Mwanza ndio kituo cha
kwanza nje ya Dodoma, ambacho Lowassa, ameanza kampeni yake ya kusaka
wadhamini.
Picha
ni, Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, ambaye tayari amechukua
fomu za kuomba CCM imteue kuwania urais, Edwrad Lowassa, akipungia
mkono maelfu ya wanachama wa chama hicho na wananchi wengine baada ya
kupata wadhamini kwenye ofisi ya CCM wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza
Ijumaa Juni 5, 2015.
Lowassa,
akipokea fomu za wadhamini ambazo tayari zimejazwa na wana CCM wilaya
ya Ilemele, kutoka kwa Katibu wa CCM wilayani humo, , Loti Olele Mtui Lazaro
Mmoja wa madereva Texi, akionyesha bango la kumuunga mkon o Lowassa, katika safari ya matumaini 2015
Lowassa, akionyesha fomu ambayo tayari imejazwa na wadhamini wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza
No comments:
Post a Comment