Friday, June 5, 2015

Jokate na Alikiba Sio MAKOMBO Tena.......Wazidi kuuweka hadharani uhusiano wao, mashabiki waupa tick


Alikiba na Jokate Mwegelo wanaendelea kukusogeza karibu katika muungano wao wa hivi karibuni. 
 
Wawili hao wanaonesha kuelemewa na uzito wa penzi lao kiasi cha kuanza kujiachia na kuualika ulimwengu kwenye dunia yao mpya.

Jokate amepost picha Instagram akiwa na hitmaker huyo wa Chekecha na kuandika:All The Best Chèr.
 
Mashabiki wanaonekana kuufurahia uhusiano huo na wengine wanasema wanapenda kuwa pamoja.
 
“Oooh wowww nina vyo wapenda hadi raha , yani couple yenu ina vutia sana , maana nyiote wazuri alafu mna jitambuwa , na atakae kuwa kinyume na hili ata kuwa hawatakii wema , maana wana damu tuliumbiwa tuwe wawili ili kusaidiana mambo mengi katika maisha, so nawapendeni sana @jokatemwegelo ,@officialalikiba , nawaombea sana Mungu azidi kuwa lindia mausiano yenu , mufike kwenye malengo mazuri zaidi, msisikilizi ya walimwengu hawana mema hawana mema,” ameandika alinezinta.

No comments:

Post a Comment