Vijana watakiwa Kuwaepuka Wanasiasa Matapeli
VIJANA
wilayani Tarime wametakiwa kuepuka baadhi ya wanasiasa wanaowatumia na
kuwafanya kuwa daraja la kupandia ili kupata vyeo kwa maslahi yao
binafsi.
Kauli
hiyo ilitolewa hivi karibuni na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Mfaume Ally Kizigo, wakati wa ziara yake
ya kuhamasisha uhai wa chama wilayani Tarime.
Alisema kuna haja vijana kuepuka wanasiasa wanaowatumia kwa maslahi yao binafsi, huku wakiwaacha mitaani wakitaabika.
Aliwatahadharisha
kabla ya kujiunga na chama chochote cha siasa wafanye upembuzi wa kina
kuangalia kitakachowavusha badala ya kukimbilia vyama kwa ushabiki.
Alisema baadhi ya vijana wamekuwa wakikimbilia vyama vya upinzani kwa ushabiki, jambo ambalo huwarudisha nyuma kimaendeleo.
“Fanyeni
utafiti kabla ya kujiunga na chama chochote cha siasa, ukijiunga na
chama kwa kufuata mkumbo mwisho wa siku utajutia,” alisema Kizigo.
No comments:
Post a Comment