Membe Akanusha kuwa na Undugu wa Damu na Kikwete
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe
amekanusha uvumi ambao umekuwa ukienezwa kuwa yeye na Rais Jakaya
Kikwete ni ndugu wa damu.
Membe amesema kuwa japo wanafanana kwa sura lakini hawana uhusiano wowote wa kibaiolojia.
Mhe.
Membe alikanusha uvumi huo jana Mjini Dodoma wakati akichukua fomu za
kuwania urais kwa tiketi ya CCM, ambapo pamoja na mambo mengine alisema
ataimarisha viwanda vidogo na vya kati.
Kada
mwingine wa CCM aliyechukua fomu za kuwania urais hii jana ni Mbunge wa
Kisesa Luhaga Mpina ambaye amesema vipaumbele vyake vitakuwa ni
kuboresha ukusanyaji wa kodi pamoja na usimamizi thabiti wa mapato ya
kodi ili taifa liondokane na utegemezi
No comments:
Post a Comment