Friday, June 5, 2015

DIAMOND ABANWA KUMSALITI MEMBE


Musa mateja
Nimwendo wa kutangaza nia kwa baadhi ya wanasiasa ambao wanaomba ridhaa ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu ambapo upepo huo umemgusa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ baada ya kwenda kufanya shoo wakati Waziri Mkuu Mjiuzulu, Edward Lowassa akitangaza nia mwishoni mwa wiki iliyopita.
Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi, Benardi Memba akiwa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
TUHUMA ZA USALITI
Mara baada ya Diamond kuangusha bonge la shoo kwenye ‘iventi’ hiyo ya kuanza Safari ya Matumaini ya Lowassa akiungana na wasanii wengine kama Tunda Man, Khadija Kopa, Makomandoo, Nay wa Mitego, Dully Sykes na wengine kibao ndipo madai mazito yakaibuka kuwa amemsaliti mtangaza nia mwingine, Bernard Membe.
TEAM MEMBE MZIGONI
Mara baada ya ishu hiyo, kundi la siri linalojiita Team Membe kwenye Mitandao ya Kijamii ya Instagram, Twitter, Facebook na WhatsApp linalodaiwa kumuunga mkono waziri huyo wa Mambo ya Nje ya Nchi, Memba walianza kutoa vitisho kwa Diamond kuwa watamshikisha adabu kwa kuisaliti kambi yao.“Hakuna asiyejua kama Diamond alikuwa ni Team Membe. Kitendo cha kwenda kumsapoti Lowassa ni usaliti.
ETI WAMETOKA MBALI?
“Sisi (Team Membe) tunajua vitu vingi. Tunajua ukaribu wa Membe kwa Diamond na namna ambavyo amekuwa akimpa sapoti. Ukweli tumeshtushwa kumuona jamaa kwa Lowassa,” ilisomeka sehemu ya maoni ya mmoja wa memba wa Team Membe na kuungwa na mwingine:
Diamond akiongozana na waziri Membe.
“Hata kipindi kile (mwaka jana), Membe alimpa shavu la shoo Mtwara na Lindi na zaidi sana akamkaribisha hotelini wakala chakula pamoja kwa lengo la kujipanga namna ya kusapotiana.“Kuna madai kwamba walikubaliana kwamba Membe atamsaidia kwenye kuupaisha muziki wake kimataifa naye akamuahidi kumsapoti kwenye siasa hasa atakapotangaza nia kwa sababu Diamond ana ushawishi mkubwa ndani na nje ya Bongo.”
WANAMTISHAJE?
Kwa mujibu wa taarifa hizo za mitandaoni, vitisho hivyo vimekuwa vikifanywa kwa maneno tu katika kurasa za Diamond lakini siyo uso kwa uso kwani bado kundi hilo ni la siri.
DIAMOND ANASEMAJE JUU YA SAKATA HILI?
Baada ya kujikusanyia data hizo ambazo ndizo habari ya mjini kwa sasa hasa ikizingatiwa Membe naye atatangaza nia ya kutaka kuwania urais kesho Jumamosi, gazeti hili lilimtafuta Diamond ambapo alitoa waraka mzito:
“Kwanza kabisa watu wanatakiwa kufahamu kwamba mimi sina chama na wala siko upande wowote.
“Yeyote atakayechaguliwa na kuonekana bora kwa wananchi basi mimi kwangu ni sawa maana sina ufahamu mzuri wa siasa kujua yupi anafaa kuliko mwenzake.
Lowasa akihutubia kwenye safari ya matumaini.
“Ila wananchi wanatakiwa kufahamu kuwa mimi ni mwanamuziki na kazi yangu ni kuburudisha…hivyo yeyote atakayeniita kwenye hafla yake niburudishe na akafikia matakwa ya malipo yangu basi siwezi kuacha kwenda.“Hivyo nawataarifu wagombea na viongozi wote…mimi ni mwanamuziki wa Tanzania na nipo kwa ajili ya kuwatumikia kiburudani Watanzania wote…. Yeyote atakayetaka nimpatie burudani basi awasiliane na uongozi wangu.”
VIPI KUHUSU VITISHO?
Alipoulizwa juu ya vitisho kutoka kwa kundi lolote, Diamond alisema hajavipata lakini endapo atapata itabidi akaripoti polisi kwa usalama wake.
TUJIKUMBUSHE
Mapema mwaka jana Diamond alialikwa na Membe kwenye shoo za kuhamasisha amani huko Mtwara na Lindi ambapo baada ya shoo alipata fursa ya kula chakula pamoja na mheshimiwa huyo. Huo ndiyo ukawa msingi kwamba staa huyo yupo upande wa Membe.
Diamond akitumbuiza.
Hata hivyo, katika maelezo yake, Diamond alikiri kufanya mazungumzo na Membe. Mazungumzo ambayo alidai yalihusu pongezi jinsi anavyojituma na kuitangaza Tanzania.Alisema pia waziri huyo alimuahidi kumpa sapoti kwa kumtafutia shoo nyingi za nje ya nchi huku Diamond yeye akiishia kuisihi serikali kuweka nguvu kwenye Muziki wa Bongo Fleva unaoajiri kundi kubwa la watu.
TUKIRUDI KWA WATANGAZA NIA
Mbali na Lowassa na Membe, wengine ambao wametangaza nia katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni pamoja na Steven Wasira, Mwigulu Nchemba, Profesa Mark Mwandosya, Luhanga Mpina, Profesa Mark Mwandosya, Fredrick Sumaye na wengine kibao.

No comments:

Post a Comment