TUNAWEZA KUIMALIZA MALARIA - RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE
Na Mwandishi Maalum, New York
Rais
Mstaafu wa awamu ya Nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amesema, anaimani
kubwa kwamba ushirikiano uliopo baina ya serikali mbalimbali barani
Afrika, mashirika ya kimataifa, makampuni binafsi na kila mtu katika
nafasi yake, hapana shaka ugonjwa wa malaria unaweza kumalizwa kabisa.
Mhe.
Kikwete ameonyesha matumaini hayo jana( alhamisi) wakati wa hafla ya
kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa jitihada
za kuutokomeza ugonjwa wa malaria ( Malaria No More) zilizoanzishwa
na Bw. Ray Chambers akishirikiana na Bw. Peter Chernin.
Katika hafla
hiyo na ambayo mshereheshaji alikuwa Bw. Wolf Blitzer mtangazaji
maarufu wa Televisheni ya Kimataifa ya CNN kupitia kipindi chake
cha situation Room, Rais mstaafu alitunukiwa tuzo
ijulikanayo kama White House Summit Awards ikiwa ni kutambua uongozi
wake, kujitoa kwake na kubwa zaidi kusimamia uanzishwaji wa muungano
wa viongozi wa Afrika dhidi ya Malaria ( ALMA) muungano ambao hadi
sasa una viongozi 49.Wengine waliotunukiwa tuzo hiyo ni Bw. Ray Chambers na Sumitomo Chemical.
Akijibu
swali la nini anadhani kumechangia katika kupunguza idadi ya vifo
vitokanavyo na ugonjwa wa malaria. Rais mstaafu amesema, zipo
sababu kadhaa, lakini kubwa ni utashi wa kisiasa wa kusimamia na
kuongoza mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Akawaeleza
wageni zaidi ya 250 walioalikwa wakiwa ni wawakilishi wa makapuni na
mashirika mbalimbali yanayochongia juhudi za kuukabili ugonjwa wa
malaria. Kwamba, Upatikanaji na usambazani wa dawa sahihi za kutibu
ugonjwa wa malaria, utengenezaji, usambazaji na matumizi ya vyandarua
vyenye viatilifu na unyunyiziaji wa dawa za kuuwa mazalia ya mbu ni
mambo ya msingi ambayo yamechangia katika kupunguza vifi vya watoto
chini ya miaka mitano.
“mchanganyiko
wa mambo hayo matatu umesaidia sana kupunguza idadi ya watoto
wanaofariki kwa malaria, lakini pia matumizi ya vyandarua vyenye
viatilifu ambapo zaidi ya vyandarua milioni 24.2
vimesambazwa, kumechangia
wanafunzi kuendelea na masomo yao bila kukatishwa mara kwa mara sababu
ya malaria, halikadhalia nguvu kazi imeimarika”. akasisitiza Rais
Kikwete na kushangiliwa na wageni waalikwa.
Mwanzilishi wa Malaria no More, Bw Peter Chernin akimkabidhi Mhe. Rais
Mstaafu, Kikwete tuzo ya White House Summit Awards ikiwa ni kutambua na
kuthamin mchango na uongozi wake katika jitihada za kuukabili ugonjwa
wa malaria, wengine waliopewa tuzo hiyo ni Bw. Ray Chambers na Kampuni
ya Sumitomo Chemical ambayo imejenga kiwanda cha vyandarua cha A-Z
Arusha Tanzania.
Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akielezea juhudi zilizofanywa
na serikali ya Tanzania katika kuukabili ugonjwa wa malaria, ilikuwa
wakati wa hafla ya miaka 10 ya Malaria no More iliyofayika jana alhamis
New York Marekani, Mhe. Kikwete amealikwa katika hafla hiyo kutokana
na mchango wake mkubwa katika pamoja na mengin kuwahamasisha viongozi
wa Afrika kuongeza juhudi za kisera, kimkakati na bajeti hali ambayo
imechangia sana katika kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano.
pamoja naye ni Bw. Peter Chernin, Bw. Ray Chambers na mwezeshaji, Bw.
Wolft Blitzer wa CNN.
Mhe. Rais Mstaafu katika mkutano na Bodi mpya ya Malaria no More muda
mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya miaka 10 ya Malaria No More.
Sehemu ya Wageni zaidi ya 250 kutoka masharika na makampuni mbalimbali
ambako ni sehemu ya wadau wa kubwa wanaochangia juhudi za kutokomeza
na kudhibiti ugonjwa wa malaria.
Burudani pia ilikuwapo.
No comments:
Post a Comment