Monday, March 28, 2016

HIVI NDIVYO Mziki wa Tanzania Unavyokuwa Kwa Kasi na Kuelekea Kuipita Nigeria


Na Amin Amali
Muziki wa Tanzania umekua kwa kiasi kikubwa tofauti nazamani, huwezi kukosa kumtaja Diamond katika muziki wa Tanzania haswa katika mafanikio kuaanzia kwake, lakini pia huwezi kukosa kumtaja Alikiba kama asingetaka kupunzika mwaka 2008 nadhani yeye ndiyo angeutoa muziki lakini bado nafasi ya Dimond ni kubwa mno.

WAPI WA NIGERIA WALIPO TUPITA HAPO AWALI?
Waliwahi kuwekeza japo muziki wao unategemea zaidi mdundo, hawakuwa na ‘melody’ nzuri wala tungo nzuri, Nigeria hawatuwezi hata kidogo  kimuziki haswa mashairi ,melody na tungo .

Wenzetu waliwekeza zaidi katika “VIDEO”baada ya kupata mdundo(beat) nzuri japo mashairi ya kawaida waliwekeza katika video na hii ili wanyanyua sana wakati sisi tulikuwa katika “Audio”
Wakati wao wako katika ‘Social media’ sisi tulikuwa bado hatujaingia sawa sawa nahii nathubutu kusema mafanikio makubwa ya Dimond kushinda tuzo mbali mbali social media

Ushirikiano pamoja na yote wenzetu hawakuwa na ubinafsi katika kushirikiana na kusaidiana tangu zamani,mfano mzuri 2face idibia ambapo kwa sasa anaitwa 2baba yeye ndiye ameitambulisha nigeria vizuri lakini hakuwa mgumu kuwapa ushirikiano wenzake.

WAPI TUMEWAPIGA BAO?
Baada ya kugundua kuwa kutoa Audio bila video ni sawa na bure kabisa hivi sasa kila msanii anawekeza katika Video kali siku akitoa audio ana toa na video.
kiswahili kutumika vizuri kimataifa hii pia ni sababu ya muziki wetu kukua na kuanza kupigwa sehemu mbali mbali duniani hii imetuongezea  wigo.

KIPI KIMEBAKI TUWE NAMBAOJA?
kitu kilicho baki ni kimoja tu wa bongo tuna‘figisu figisu’ sana katika kushirikiana , tukitekeleza kupendana na kushirikiana sawa sawa Nigeria itakuwa namba mbili kumbuka hapo awali  Afrika kusini walikuwa namba moja kabla ya Nigeria kuchukua hatamu na kama inavyo endelea kwa sasa tunaenda kuwa namba moja

No comments:

Post a Comment