Fidel Castro akosoa ziara ya Obama Cuba
Aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu wa
Cuba Fidel Castro amevunja kimya chake kuhusu ziara ya hivi majuzi ya
Rais wa Marekani Barack Obama nchini humo.
Kwenye barua iliyochapishwa katika gazeti la serikali ya nchi hiyo la Granma kiongozi huyo ameonekana kukosoa ziara hiyo.Fidel, aliyemkabidhi kakake Raul uongozi wa taifa hilo mwongo mmoja uliopita, amesema Cuba haihitaji zawadi zozote kutoka kwa Marekani.
Obama na Castro wajibizana Cuba
Amesema maneno ya Obama ya kuhimiza maridhiano ni sawa na “rojo ya sukari” na kuonya kwamba raia wa Cuba wanaweza kupata “mshtuko wa moyo”.
Fidel Castro, 89, aliongoza Cuba kuanzia 1959 hadi 2008 alipomkabidhi nduguye madaraka.
imetolewa na Neema jr
No comments:
Post a Comment