Dogo Janja: Shule Sio Kitu cha Kufanya Kwa kuiga, Siitaki Tena (Video)
“Msomi Nick wa Pili, mimi niliachaga Makongo,” anasema Dogo Janja kwenye wimbo wake mpya, My Life.
Na sasa rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa hawezi tena kurudi shule.
“Siku zote linapokuja suala la elimu, sio kitu cha kufanya kwaajili ya kuiga na pia unatakiwa ufuate kichwa chako kinaenda vipi. Sometimes watu wanaweza wakawa wanakuforce sana ‘soma, soma’ lakini wewe mwenyewe unakuwa unaangalia future yangu mimi haipo kwenye kusoma,” amesema.
“Au hata nikipelekwa kusoma, siwezi nikafanya vizuri, kwahiyo ni bora ukomboe hela za watu wanaotaka kukusaidia kukupeleka shule,” ameongeza.“Kama kuna kitu cha kusomea nitasoma, lakini sio ile elimu ya kuvaa masare, kukimbia pale getini pale Makongo, kutembea na mguu, Mwenge to Makongo, hapana siwezi.
No comments:
Post a Comment