Ustaa na Umaarufu wa Ghafla Wamfanya Mwanamuziki Ruby Kubadili Mpenzi...wa Mwanzo Amwagwa
Ruby star wa muziki ambaye ujio wake umekuwa ni wa kishindo kikubwa katika tasnia ya muziki wa Bongo Flava, ametufungulia moyo wake na kuweka wazi namna ambavyo safari yake katika usupa star imebadilisha kabisa mahusiano yake ya kimapenzi.
Kwa taarifa ambayo eNewz inakupa wewe kwa mara ya kwanza kabisa, The Beautiful Ruby ambaye offcourse maisha yake yamebadilika na yanaendelea kubadilika kwa kasi, amelazimika pia kubadili mahusiano yake ya kimapenzi ambapo kwa sasa anatoka na mtu mpya na wanaelewana na kwenda sawa bila kumuweka wazi hasa ni nani huyo.
Ruby ameeleza kuwa, mahusiano yake haya mapya yamemfunza kujishusha na kuwa mfano bora kama kioo cha jamii, huku akifurahia zaidi umaarufu wake kutia nakshi zaidi mahaba katika mahusiano hayo mapya.
No comments:
Post a Comment