Lungi Maulanga alizwa na vibaka
Msanii wa Bongo Movie nchini, Lungi Maulanga amejikuta akilizwa na vibaka baada ya kuibiwa baadhi ya vitu vya ndani wakati akiwa katika mtoko wa usiku hali ambayo imemtia hasara na kumrudisha nyuma kimaendeleo.
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa msanii huyo amedai kuwa tukio hilo
lililotokea maeneo ya Magomeni, jijini Dar es Salaam limempa Lungi hasara kwani kitendo hicho ni kurudishana nyuma kimaendeleo.
Lungi amekiri kulizwa na vibaka hao na kusema kuwa amechoka sasa
kwani sio mara ya kwanza kufanyiwa kitendo kama hicho na kusema kuwa
anajiandaa kuhama ili kukwepa adha hiyo na kudai kuwa ameibiwa vitu
kadhaa ikiwemo Tv na deki.
No comments:
Post a Comment