Tamaa ya Kuwa na MAKALIO Makubwa Yamsababishia Kifo Msichana Huyu Mrembo
Tunashuhudia watu wengi wakiongeza makalio kwa kusudi la kuwa wenye mvuto zaidi, na kumekuwepo na vidonge na sasa kuna sindano za kuongeza makalio.
Leo nimekutana na stori iliyotokea Los Angeles Marekani, ambako msichana Kelly Mayhew mwenye miaka 34 amefariki baada ya kufikishwa St.John’s Espiscopal Hospital, muda mfupi baada ya kuchomwa sindano ya kuongeza makalio.
Kelly Mayhew na mama yake walisafiri kutoka Maryland kwenda Rockaway, walikokua wameelekezwa na rafiki yake Kelly ili kwenda kuchoma sindano hiyo ambayo ilikua inatolewa kinyume na utaratibu… mtoaji wa huduma hiyo alijiita daktari lakini hakuwa amesajiliwa na alikuwa hatambuliki kisheria.
Baada ya kuchomwa sindano hiyo, Kelly alianza kupumua kwa shida, akawa anajitupa ovyo chini huku akiishiwa pumzi… baada ya kuhangaika kwa kama dakika ishirini hivi, Kelly alifariki akiwa kwenye mikono ya mama yake.. mpaka Polisi wanafika eneo hilo Daktari alikuwa tayari kashakimbia.
No comments:
Post a Comment