Wednesday, May 20, 2015

Huddah The boss chick amesema kuwa kamwe hatakuja kumuanika mpenzi wake kwenye mtandao wa kushare picha wa Instagram, kwa kuhofia kinadada wajanja wasije kumrubuni na kumnkurunziza kumpindua.

Mrembo huyo kutoka Kenya licha ya kuwa amewahi kushare picha za mwili wake ukiwa mtupu kabisa, amesema kuwa miongoni mwa vitu ambavyo hawezi kushare na followers wake zaidi ya laki 2, ni mpenzi wake, nyumbani kwake, kitanda chake pamoja na ndugu zake kwasababu huo ni upande wa maisha yake binafsi.

“Never! That is my private. Nyumba yangu, boyfriend wangu, mahali naweka kichwa nalala, utaona tu hotel niko vacation and all that, lakini mahali naweka kichwa changu nalala, na mtu aliyeuteka moyo wangu ni vitu ambavyo kamwe siwezi kuweka Instagram, hata familia yangu siwezi kuwaweka Instagram.” Alisema Huddah kupitia Amplifaya ya Clouds Fm.


Ameongeza kuwa picha nyingi ambazo huwa anaweka huwa ni za hotelini pamoja na zake mwenyewe, na haweki picha za mpenzi wake kuhofia wasichana wa mjini wasije kumrubuni na kumpora.

Huwa naweka zangu tu, watu wanaona mimi mbinafsi kwasababu huwa siweka picha za watu wengine, kwasababu Instagram ina watu wengine wana matusi sana, wakati mwingine unaweza kuweka picha na rafiki yako wanamtusi rafiki yako, sasa imagine uweke mtu kama boyfriend wako halafu tena wasichana wana competition, wakiona ooh huyu ndio boyfriend wa Huddah, wanataka kumfatilia yule jamaa wanam Dm Dm huko ndani picha uchi zingine halafu bado wanakuja kunitusi, I don’t put my private life out there”.
Udaku Special Blog

No comments:

Post a Comment