Majambazi wamevamia nyumba ya Ali Kiba usiku wa kuamkia leo, picha na taarifa za mwanzo viko hapa
Reporter wa millardayo.com alikuwa mmoja ya watu wa kwanza kupewa taarifa juu ya tukio hili, akafika Kunduchi Dar es salaam ambako Ali Kiba na mdogo wake Abdu Kiba wanaishi.
Nimeongea na Abdu Kiba, amesema yeye alikuwa Masaki, Ali akampigia simu kwamba kuna watu kama 15 hivi wamevamia nyumbani kwao..
waliovamia waliruka ukuta saa tisa usiku, wakavunja mlango wa sebuleni,
wakakuta vijana wawili ambao wanaishi nao, wakawapiga na kuwalazimisha
wawaoneshe chumba ambacho Ali yumo.. wale vijana wakajibu kwamba Ali hayupo, wakaulizia chumba chake wakaoneshwa chumba cha Abdu Kiba.
Wameingia chumbani wakamkosa Ali Kiba, wameiba vitu vingi vya sebuleni na chumbani pia, pamoja na pesa milioni 2 na nusu zilizokuwa chumbani kwa Abdu.
Abdu amesema alitoa taarifa Polisi, wakafika usiku huo huo na kuanza ukaguzi wa eneo lote la nyumba.
Imenifikia SASA hivi: Nyumba ya akina ALI KIBA imevamiwa usiku wa kuamkia leo, naifuatilia na ishu yote nakuletea on http://t.co/G3BpafI2ae.
— millardayo.com (@millardayo) May 2, 2015
Wakati tukio lote linaendelea Ali alikuwa ndani kwenye chumba kingine, hawakuomuona.
No comments:
Post a Comment