Kigogo Mpya Wa Jack Wolper Anaswa
Achilia mbali akina pedeshee Mangi, Dallas na Gee Modal, kigogo mpya wa staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe safari hii amenaswa laivu wakijiachia kwa raha zao.
Kwa mujibu wa chanzo, kigogo huyo ni mtu mwenye
fedha zake aitwaye Jimmy Mgaya ambaye ni Mbongo mfanyabiashara aishie
nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.
Chanzo hicho kilishusha data kuwa jamaa huyo ndiye aliyempangia
Wolper nyumba ya kifahari iliyopo ushuani Mbezi-Beach jijini Dar.Huku
akirusha picha za kimahaba za wawili hao, sosi wetu huyo alisema kuwa
Jimmy ni ‘mtu f’lani hivi amazing’ kwa sababu anakata mkwanja kinoma.
Chanzo hicho kilidai kwamba picha za wawili hao wakijiachia zilipigwa maskani kwa jamaa huyo huko Durban
kwenye Jimbo la KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini.
Baada ya jitihada za kumsaka mwanaume huyo kugonga mwamba, Wolper alipigiwa simu na kusomewa mashitaka yake juu ya mwanaume
huyo ambapo mbali na kukiri kumfahamu Jimmy, alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli namfahamu Jimmy, nilikutana naye kwenye mizunguko yangu nje
ya nchi. Si kweli kwamba ni bwana’ngu. Kuhusu picha, nilipiga naye kama
rafiki tu na sioni kama ni picha mbaya.”
Hivi karibuni Wolper alikiri kuwa na mwanaume lakini akawa anaogopa
kumwanika kwa kuogopa kuporwa na wasichana wa mjini hivyo inaaminika
ndiye huyo Jimmy.
No comments:
Post a Comment