Friday, July 10, 2015

Mpasuko CCM: Nchimbi, Sophia Simba na Adam Kimbisa Wapinga Jina la Edwarad Lowassa Kukatwa


Habari za Hivi punde kutoka makao makuu ya CCM mkoani Dodoma  ni kwamba wajumbe wa kamati kuu  watatu ambao ni  Dkt. Emmanuel Nchimbi, Sophia Simba na Adam Kimbisa  wamepinga maamuzi ya kamati ya kumkata mmoja wa wagombea maarufu   na kumweka mgombea asiyekuwa maarufu.
 
Akizungumza usiku huu majira ya saa saba za usiku Dkt. Nchimbi amesema kwamba wao watatu hawajakubaliana na maamuzi ya kamati kuu iliyoketi usiku huu chini ya Mwenyekiti Dkt Jakaya Kikwete kumkata mgombea maarufu kwa manufaa ya mgombea asiye maarufu.
 
“Katika kikao cha leo kamati haikupoea majina yote yaliyojadiliwa na maadili, suala ambalo ni kinyume na kanuni, pili katiba ya CCM inataka mtu anayekubalika  ndiye apewe nafasi ya kwanza, lakini kikao cha leo kimeonyesha kuminya wanaokubalika  kwa manufaa ya wachache wasiokubalika” Amesema Dkt. Nchimbi.
 
Hivyo basi kwa sababu hiyo wao watatu ambao ni wajumbe wa kamati kuu wamewataarifu wenzao  kwamba wamejitenga na maamuzi ya kikao hicho na kutangaza kuto kuyaunga mkono.
 
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kisiasa nchini Tanzania zinaonesha kuwa mgombea anayekubalisa sana CCM ni Mbunge wa Monduli Edward Lowassa akifuatiwa na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa  Bernad Membe.

Hapo  chini  nimekuwekea  Video  ya  Emmanuel  Nchimbi  akiyapinga  maamuzi  hayo.
 

No comments:

Post a Comment