MWANZA : Takukuru yawaburuza kortini vigogo watatu wa Serikali
R D PRODUCTION
TAASISI
ya Kupambana na Kudhibiti Rushwa nchini (TAKUKURU) imewaburuza
mahakamani vigogo watatu wa Serikali kwa makosa mawili ya matumizi
mabaya ya madaraka na kutumia nyaraka mbalimbali kumtapeli mwajiri
wao.
Vigogo
hao ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mkoa wa
Shinyanga, Patrick Karangwa (45), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Magu Mkoa wa Mwanza, Ntinika Paul (51) na Mhasibu Mkuu wa Wilaya ya
Magu, Mathayo Masuka.
Walifikishwa
wiki iliyopita katika Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza,
mbele ya Hakimu Mkuu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Janeth Masesa.
Ilidaiwa kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa hayo mwaka 2009 wakati wakiwa wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Ilielezwa
kuwa wakati wakitenda makosa hayo, Karangwa alikuwa Mchumi Mkuu Jiji la
Mwanza, Paul alikuwa mweka hazina mkuu wa jiji hilo wakati Masuka
alikuwa mkaguzi wa ndani wa jiji la Mwanza.
Watuhumiwa hao walikana mashtaka hayo na wapo nje kwa dhamana na kesi hiyo inatarajiwa kutajwa tena Juni 11 mwaka huu.
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza, Kasomambuto Mbengwa, alithibitisha taasisi hiyo kuwakifikisha vigogo hao mahakamni.
Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment