Sunday, June 7, 2015

Mama amchoma mikono mwanae kwa madai ya kuiba ugali

Mpekuzi blog

Stamili Mponzi mkazi wa kijiji cha Ikule wilayani Kilombero,  mkoani Morogoro anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumchoma mwanae na kumjeruhi mikono kwa madai ya kuiba ugali.

Mama huyo alimuunguza mwanaye  Joseph Chawala, akimtuhumu Kuiba Ugali, kwa mujibu wa watendaji  mbalimbali wa kata ya Mng’eta.
 
Wakizungumzia tukio hilo Jerome Chulu na Jeneth Hetela,  walisema unyanyasaji huo  ulishuhudiwa na majirani wa mwanamke huyo baada ya kusikia kelele za watoto ambao walimchukua mtoto huyo kumpeleka ofisi  ya mtendaji wa kata,polisi na baadaye hospitali.

Walibainisha baadaye kuwa polisi  walikwenda kumkamata mwanamke huyo na mumewe Halidi Kiwenji ambaye  inadaiwa alikuwa karibu wakati wa tukio hilo ingawa baadaye baba huyo aliachiwa ili akawaangalie watoto wengine nyumbani.

Polisi  walithibitisha tukio hilo ambalo uchuguzi wake unaendelea ili kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo.
 
Wananchi mbalimbali waliohojiwa wametaka hatua kuchukuliwà kwa watu wanaoendekeza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
 
POSTED BY. RASHID HAMZA

No comments:

Post a Comment