Tuesday, June 23, 2015

Kuna watu hawajaisahau ishu ya wanyama kutoroshwa kutoka Hifadhi za wanyama TZ, hii imetokjea Bungeni Dodoma leo June 23 2015 (Audio)


GiraffeIshu ya wanyama kutoroshwa TZ iliingia kwenye headlines na kusababisha baadhi ya Mabadiliko kwenye Baraza la Mawaziri ikiwemo aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii kusimamishwa kazi… hii ishu wapo walioisahau na wapo ambao hawajaisahau kabisa.
Imerudi tena ndani ya Kikao cha Bunge leo June 23 2015 >>> “Wakati tunamuwajibisha Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Ezekiel Maige kwas sakata la utoroshaji wa Wanyamapori, Wizara ilisema itaunda Tume ya Uchunguzi kwenda Qatar kuchunguzana Tume hii iliunda, nataka kujua kwa nini Tume hii isiende Qatar na mpaka sasa Serikali imekaa kimya“>>> Christowaja Mtinda.
Serikali kukiri tukio hili kutokea kwenye Uwanja wa Ndege na inakuja na mkakati wa kuimarisha Ulinzi katikaViwanja vua ndege, wakati wanyama wanatoroshwa ina maana Viwanja vya Ndege havikuwa na Ulinzi?”>>> Christowaja Mtinda.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii akaja na majibu haya >>> “Kuna tatizo limetokea, kukiri ni uungwana lakini kuna hatuatumechukua kuhakikisha tatizohalizoteki tena ikiwemo kufukuza wahusika wote
Iliundwa Tume, tulifanya Uchunguzi na kazi inaendelea, kwa mujibu wa Sheria kwenda kwenye nchi nyingine ni mpaka tupate kibali kwa hiyo tunashughulikia kupata kibali kwenda Qatar”>>> Mohamed Mgimwa.
Iko stori hiyo pia kwenye sauti hii mtu wangu toka kwenye Kikao cha Bunge Dodoma.

No comments:

Post a Comment