Tuesday, June 30, 2015

Membe Arudisha Fomu Ya Urais......Akana Kuhusika Na Ufisadi Wa Mabilioni Ya Libya.


MAKADA maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamerejesha fomu na kufafanua mambo kadhaa ambayo yamekuwa yanazungumzwa juu yao kama njia ya kujiweka sawa kabla ya uteuzi kufanywa na vikao vikuu vya chama hicho.
 
Mmoja wa waliorudisha fomu ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye wakati akirudisha fomu za kuomba kuteuliwa na kusema kuwa wanaochukulia suala la urais ni la kufa au kupona wana matatizo kwani anayejua Rais wa Tanzania ajaye ni Mungu.
 
Alisema safari yake ya kutafuta wadhamini ilikuwa na misukosuko mingi ikiwemo kutokea ajali tatu lakini hakuna ambaye alikuwa ameumia sana.
 
Akiwa ameongozana na mke wake, Tunu Pinda alisema mwana CCM mkomavu ni yule ambaye yuko tayari kukubali matokeo.
 
Alisema mpaka sasa ni wanachama wa CCM 42 waliojitokeza kugombea lakini katika hatua ya kwanza ni majina matano tu yatakayoteuliwa na kundi kubwa litaondolewa.
 
“Mimi sitegemei kwenye mchujo wa watu watano watokee watu wa kunung’unika kwani kila mtu aliyefika kuchukua fomu alikuwa anafahamu kuwa kutakuwa na mchujo kama tuko wengi wako watano kisha unakwenda ngazi ya pili, hakuna sababu ya kunung’unika,” alisema.
 
Alisema baadaye kuna kwenda kwenye Mkutano Mkuu atabaki mmoja. “Utanung’unikia nini? Kuna kushinda na kushindwa na kuna kupata na kukosa na ukisema suala la Urais ni kufa au kupona basi una matatizo, ifike mahali wana CCM wapate mtu ambaye wanadhani anaweza kusaidia kuongoza,” alisema.
 
Pia alisema waliojitokeza mwaka huu kuchukua fomu ni wengi. “Tuliojitokeza tusinuniane, kwa nini haniungi mimi mkono, na wewe usione jambo hili ni nongwa na usijione mapenzi ya Mungu yako kwako tu,” alisema.
 
Pia aliwataka viongozi wenzake washirikiane kumuunga mkono mgombea mmoja atakayepeperusha bendera ya CCM. “Anayejua rais wa Tanzania atakuwa nani ni Mungu peke yake,” alisema.
 
Mwakyembe arudisha fomu
Waziri wa Afrika Mashariki, Dk Harrison Mwakyembe jana alirudisha fomu na kusema CCM itapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu kutokana na kutekeleza ilani yake vizuri na wananchi kuwa na imani kubwa na chama hicho.
 
Mwakyembe ambaye alirudisha fomu jana mchana alisema katika safari yake ya kutafuta wadhamini mkoani ameweza kuwaona wanachama wengi wa CCM ambao wanaonesha imani kubwa na chama chao.
 
Alisema kila alipokutana na wana CCM waliojitokeza kumdhamini kwa tathmini aliyofanya tangu kuanza kwa siasa ya vyama vingi nchini CCM, itashinda ushindi wa kimbunga kwani mtaji upo kutokana na kazi kubwa iliyofanya serikali ya awamu ya nne katika utekelezaji wa ilani.
 
“Tumejipanga kuhakikisha wanaingia kwenye uchaguzi kifua mbele kutokana na kutekeleza ilani,” alisema. 
 
Pia alisema kwa upande wa pili wana kazi ya kuhakikisha yote mazuri yaliyofanywa na CCM yanasemwa.
 
 “Tuna kazi ya kuhakikisha kuwakumbusha wananchi barabara za lami na mafanikio mengi yamepatikana na serikali ya awamu ya nne ya CCM,” alisema.
 
Alisema kazi kubwa ni kuhakikisha umma unatambua CCM imefanya mambo mengi kutokana na upotoshaji unaofanywa na wapinzani kuwa CCM haijafanya lolote.
 
Pia alisema CCM kuwa na wagombea wengi waliojitokeza mwaka huu ni dalili njema za CCM kutoa fursa za kupatikana mmoja ambaye kila moja atamuunga mkono ili kuweza kukivusha chama.
 
Dk Mwakyembe alisema yuko tayari kumuunga mkono mgombea atakayeteuliwa na chama. Awali alisema amezunguka katika mikoa 15 katika kutafuta wadhamini.
 
Dk Mwele Malecela
Mwanachama mwingine wa CCM aliyerudisha fomu jana ni Dk Mwele Malecela ambaye alisema pamoja na kazi kubwa iliyofanywa katika uongozi wa awamu nne bado kuna watu wanaoishi kwenye umasikini uliokithiri.
 
Alitoa kauli hiyo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari. Alisema alifanikiwa kupata wadhamini katika mikoa 20 ikiwemo 17 ya Tanzania bara na mitatu ya Zanzibar.
 
Alisema wananchi wameonekana kufarijika kuona wanafuatwa kwenye maeneo ya kata walipo. Alisema ameweza kuzunguka mikoa tisa kwa siku nne hali inayoonesha kuwa kazi kubwa imefanyika katika ujenzi wa barabara za lami kuunganisha mikoa.
 
‘Pamoja na maendeleo na kazi kubwa ya awamu zote bado kuna umasikini uliokithiri lazima kuliangalia suala hilo kama kiongozi na kulitafutia ufumbuzi,” alisema.
 
Alisema aliguswa sana na wanawake waliojitokeza wakiwemo wazee ambao walikuwa wakitaka kumuona ni mwanamke wa aina gani ambaye anataka kugombea Urais.
 
“Wanawake wamefurahi sana kuona wanawake tunajitokeza hii ni fursa nzuri ya kuwapa moyo akinamama kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika nchi,” alisema.
 
Membe Ayakana  Mabilioni  ya  Libya
Membe kwa upande wake wakati anarudisha fomu akijibu swali aliloulizwa kuhusu madai ya kuwa anahusika na ufisadi wa fedha za Libya na kama inavyosambazwa na wapinzani wake, alisema akigundulika kuwa alikula hata dola moja yuko tayari kujiuzulu.
 
“Uvumi kuwa nahusika na mabilioni ya Libya hauna mashiko kabisa baadhi ya wanasiasa wenzangu wanajua ukweli wote huu lakini kwa makusudi wameamua kuniunganisha na kampuni hiyo na kuwaaminisha watu ni yangu au nina hisa maneno hayo ni ya uongo,” alisema.
 
Alifafanua kuwa Libya ni moja kati ya nchi wafadhili wa Tanzania ambapo, kama ilivyo wafadhili wengine imekuwa ikiipa Tanzania misaada na mikopo yenye masharti nafuu.
 
Alisema katika utaratibu huo, Tanzania na Libya zilitia sahihi mkataba wa kubadili madeni na kuyaingiza katika miradi ambao uliweka utaratibu wa matumizi na urejeshaji wa fedha za deni la Libya.
 
Alisema kumbukumbu alizonazo zinabainisha kuwa kabla ya Serikali ya Libya kuweka saini katika mkataba wa nyongeza iliyotaka fedha hizo zikopeshwe kwa kampuni ya Meis, upembuzi yakinifu wa mradi husika ulifanywa kupitia vyombo vyake, na wao wenyewe kujiridhisha juu ya ubora wa mradi huo.
 
Sumaye na mahakama ya rushwa
 Naye Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ambaye naye alirejesha fomu alisema akichagulia kuwa Rais wa nchi ataanzisha mahakama maalumu ya wala rushwa.
 
Mbali na rushwa pia vipaumbele vyake ni pamoja na ufisadi, uhujumu uchumi na kwamba ataunda chombo cha uchunguzi katika masuala hayo.
 
Pia alisema wakati akiwa Waziri Mkuu wa Tanzania alifanya mambo makubwa na atahakikisha anaunda serikali inayofahamu kutimiza wajibu wake.
 
‘Uchumi ninaouzungumzia si wa takwimu ni wa hali halisi, nitaangalia pia maeneo kama viwanda vikubwa na vidogo ili watu wengi waweze kujiajiri na kulinda viwanda vya ndani,” alisema.
 
Alisema atahakikisha uzalishaji wa viwanda vya ndani unaongezeka na kunakuwa na ongezeko la mauzo ya nje ya nchi. Pia alisema ataimarisha huduma za jamii, ikiwemo elimu, afya upatikanaji wa maji na huduma nyingine muhimu.
 
Alipohojiwa kama maeneo aliyokwenda kutafuta wadhamini aliombwa rushwa, Sumaye alisema, tangu aanze kazi ya siasa hajawahi kutoa rushwa.
 
“Hata maeneo ambayo nimekwenda kutafuta wadhamini sijatoa fedha hata zilizodaiwa kwa lugha laini nilikataa kwani nilitaka nidhaminiwe na wale walio na imani na mimi,” alisema.
 
Alisema wakati akiwa Waziri Mkuu alipambana na wala rushwa ambapo aliweza kuwafukuza kazi watu 3,360 huku wengine 400 walipelekwa mahakamani.
 
Balozi Mahiga
Balozi Mahiga naye wakati anarejesha fomu alisema ameenda mikoa 15 kwa gari na akawashukuru wana CCM kumlaki na kwamba wamehamasika na wanasubiri kwa hamu uchaguzi.
 
Alisema kama CCM ikimpitisha kuwa mgombea atahakikisha kuwa anajenga maadili ya uongozi ili kuondokana na vitendo vya rushwa na ufisadi.
 
Alisema uongozi mzuri ni ule unaojengwa katika misingi ya maadili na atapambana na rushwa ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikirudisha nyuma wananchi wengi.
 
“Nitahakikisha ninaimarisha misingi ya umoja na mshikamano katika nchi ikiwa ni pamoja na kudumisha muungano wa Tanzania na Zanzibar,” alisema.
 
Joseph Chaggama
Mwanachama mwingine wa CCM aliyerudisha fomu jana ni Joseph Chaggama ambaye alisema amezunguka katika mikoa 17 wakati wa kutafuta wadhamini. Alisema anaijua CCM vizuri na jinsi Serikali inavyoendeshwa.
 
Alisema yeye ni mmoja wa watu wasiofahamika na sababu ya kuchukua fomu ni nia ya dhati kutoka moyoni kuwa anaweza kuongoza nchi.
 
Pia alisema uwezekano wa yeye kuchaguliwa lazima kutokee muujiza. Alisema yuko tayari kuwatumikia Watanzania ikiwa atapewa ridhaa ya kuwa mgombea wa CCM na akashinda uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
 
Pia alisema yuko tayari kumuunga mkono mgombea ambaye atateuliwa na chama.
 
Monica Mbega
Mbunge wa zamani wa Iringa Mjini, Monica Mbega naye alirudisha fomu na kusema kuwa chama kiliweka utaratibu mzuri wakati wakienda mkoani kupata wadhamini katika mikoa 15 ikiwemo mitatu ya Zanzibar.
 
Alisema amekamilisha kazi yake kwa ukamilifu bila matatizo na kuwashukuru wanawake wengi waliojitokeza kumuunga mkono.
 
Alisema suala la rushwa linategemea jinsi mtu alivyokwenda wakati akitafuta wadhamini.
 
Amos akemea matumizi makubwa ya fedha
Mwingine aliyerudisha fomu hizo jana ni Amosi Siyantemi ambaye ni mtumishi wa CCM wakati ambaye alisema kuwa kwenye mchakato wa kutafuta wadhamini baadhi ya wagombea wameonesha matumizi makubwa ya fedha.
 
“Ni jambo la kujiuliza fedha hizo wamepata wapi na ni kiasi gani ni lazima wachunguzwe na kuchukuliwa hatua,” alisema Siyantemi.
 
Pia alisema rushwa ni ugonjwa mbaya unaoiangamiza jamii ni lazima zichukuliwe hatua za haraka na makusudi ili kuweza kukomesha suala hilo kabla nchi haijatumbukia kwenye shimo la machafuko.
 
Alisema CCM ya sasa si kama ile ya Mwalimu Nyerere. “Tunahitaji kurejesha haraka heshima ya CCM machoni mwa Watanzania na kwenye macho ya Jumuiya ya Kimataifa,” alisema.
 
Alisema akichaguliwa kuwa Rais atahakikisha kunakuwa na huduma bora za matibabu sanjari na bima ya afya kwa kila Mtanzania, kufanya mabadiliko makubwa kwenye mfumo wa elimu kwa kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kupunguza idadi ya masomo.
 
Pia alisema atapiga marufuku mauzo na manunuzi yanayofanyika nchini kwa malipo ya dola ambapo malipo ya dola yatafanyika kwa kibali maalumu.
 
Pia alisema atakuwa na jukumu la kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya sanaa, michezo na burudani yatakayolenga kuwanufaisha kiuchumi wananchi.

Wednesday, July 1, 2015

Nimezaa na Mose Iyobo lakini ndoa yangu ipo pale pale – Aunty Ezekiel

Mpekuzi blog

Msanii wa filamu nchini Tanzania, Aunty Ezekiel, amekiri kuzaa nje ya ndoa na kusema kuwa licha ya kuzaa nje ya ndoa bado anaamini  ndoa yake ipo palepale na mume wake Sunday Demonte.
 
Amesema kuwa ameamua kuzaa na Mose Iyobo,  dansa wa Diamond kwa kuwa muda wa kuitwa mama ulikuwa umefika.

“Mimi niliamua kupata mtoto baada ya kuona wakati umefika,” amesema.
 
“Kwasababu siku zinaenda pamoja na umri inabidi maisha yaendelee mbele. Ndoa yangu ipo kama ilivyokuwa mwanzo, haijavunjika, sijawahi kuongea kama nimezaa nje ya ndoa au ndani ya ndoa lakini mwisho wa siku ndoa yangu bado ipo,” ameongeza.
 
“Haya ni maisha na vitu vinavyozungumzwa vipo kama vilivyo, lakini familia yangu na watu wa karibu wanaelewa nini kinaendelea ndani yake na watu niliokuwa nao wanaelewa na sidhani kama itakuwa right kuongea kwenye media. Lakini watu wajue baba yake ni Mose,” amesisitiza muigizaji huyo.

Pia Aunty amewatoa hofu mashabiki wa kazi zake kwa kusema kuzaa kwake sio mwisho wa kuigiza.
 
“Kupata mtoto kwenye maisha yangu ni kitu kizuri kwa sababu kuna vitu vingi ambavyo nimepunguza na nimekuwa mama mwenye majukumu, ninapofanya vitu vyangu najua kesho na kesho kutwa kuna mtu ananitegemea. 
 
Pia kuzaa kwangu sioo kwamba kutaua sanaa yangu, sanaa yangu ipo pale pale na hata nitakapomaliza kulea nitakuwa na vitu vingi zaidi kwa sababu natumia muda mwingi kulea Kwahiyo nikirudi wategemee vitu vikubwa zaidi ingawa kuna kazi ambazo niliziandaa zitatoka wakati ninalea.”

Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano, 2015/ 2016

Mpekuzi blog

OWM-TAMISEMI inawatangazia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2015.Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali.

Jumla ya wanafunzi 55,003 wakiwemo wasichana 23,303 na wavulana31,700 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi.

 
Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 29,744 wakiwemo wasichana 11,450 nawavulana 18,294 sawa na asilimia 54.08 watajiunga na masomo ya Sayansina Hisabati; na wanafunzi 25,259 wakiwemo wasichana 11,853 nawavulana 13,406 sawa na asilimia 45.92 wamechaguliwa kusoma masomoya Sanaa na Biashara.

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2015 wataanza muhula wa kwanza tarehe 18 Julai, 2015 na hakutakuwa nafursa ya mabadiliko yoyote ya shule. 

 
Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya mwisho yakuripoti, nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi.

Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano naVyuo vya Ufundi mwaka 2015 inapatikana kwenye tovuti ya OWMTAMISEMI
ya www.pmoralg.go.tz

Imetolewa na Katibu Mkuu,


MAELEKEZO: Matokeo yanatoka kwa kituo kizima ulichofanyia mtihani.

Jinsi  Ya  Kupata kituo  chako:
Kwenye kisanduku anza kuandika jina la kituo ulichofanyia mtihani na usubiri, jina lililokamilika la kituo litajimalizia lenyewe ikiwemo namba ya kituo. 

Mfano: Iyunga, Halafu  Subiri  kidogo  ili  ijimalizie  yenyewe

Ukishachagua utabofya neno 'retrive' na utapata majina ya shule yako yote uliyotoka. 

Monday, June 29, 2015

Mapokezi ya Steve Nyerere alivyotangaza kugombea Ubunge wa Kinondoni (Pichaz)

on
Steve II
Kwenye list ya mastaa wa TZ waliotangaza kugombea Ubunge kwenye Uchaguzi wa 2015 lipo pia jina la mastaa wa Bongo Movie, Steve Mengere aka Steve Nyerere.
Jamaa alikuwa anamaanisha kabisa kuhusu safari yake kwenye Siasa, hapa nina pichaz kutoka MICHUZI BLOG ambazo zimepigwa kwenye viwanja vya CCM Bwawani ambapo Steve alikuwa akitangaza nia hiyo.
Steve III
Steve IV
Steve
Mama zangu, baba zangu, vijana wenzangu.. jitokezeni kujiandikisha ni haki yenu ya msingi hasa katika Uchaguzi Mkuu ujao… Mimi Steve Nyerere nimeamua kwa dhati kujitoa na kutangaza nia ya kuwania Ubunge wa Kinondoni“– Steve Nyerere.

  Yalichoandika magazeti ya Tanzania leo JUNE 29, 2015 Udaku, Hardnews na Michezo
Image00041
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Vote Diamond& Vanessa