Friday, May 1, 2015

Mbowe Apata Mpinzani wa Ubunge Hai


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Kilimanjaro (KNCU) Maynard Swai, ametangaza kuwania ubunge katika Jimbo la Hai kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). 
 
Kwa tangazo hilo, Swai sasa atakuwa na kibarua kizito cha kukabili upinzani kutoka kwa mbunge wa  sasa wa jimbo hilo, Freeman Mbowe (Chadema) ambaye tayari ametangaza nia ya kutetea nafasi yake katika Uchaguzi Mkuu ujao.
 
Hata hivyo, kurudi kwa Mbowe kwenye kinyang’anyiro cha ubunge jimboni humo kutategemea uamuzi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao utalazimika kumkubali au kumkataa kupitia vikao vyake vya kupanga wagombea.
 
Swai anatakiwa kupita kwenye kura ya maoni ndani ya CCM, kabla hajawa mgombea rasmi.
 
 Swai ambaye ni kada wa kwanza wa CCM kufungua pazia la kutangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Hai, alisema jana kuwa dhamira yake ni kufanya kazi na wananchi ndani ya jimbo hilo, tofauti na sasa ambapo wawakilishi wengi wanaomba kura na wakipata wanahamia Dar es Salam.
 
“Nimeamua kuingia kwenye siasa niendelee kuwatumikia wananchi. Ifike mahali kiongozi anayechaguliwa aishi na wananchi ili ajue shida zao, matatizo yao na changamoto walizonazo na siyo unapewa heshima na wananchi, lakini ukipata huonekani ukiwatumiakia,” alisema Swai.
 
Alisema iwapo chama kitampa ridhaa ya kugombea, atahakikisha anawaweka vijana pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili likiwemo suala la ajira.HUU NDI UONGOZI
CHANZO Mpekuzi blog

No comments:

Post a Comment