Friday, May 1, 2015

DIAMOND MWANANGU USISUBIRI NIFE!

Maskini! Wakati leo akiangusha pati ya nguvu na mpenzi wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ inayokwenda kwa jina la Zari All White Party kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar, baba mzazi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Jumaa yu hoi kitandani huku akimtaka mwanaye huyo kuonesha msamaha wa kweli aliotangaza kwenye vyombo vya habari na kwamba asisubiri hadi afe.
Baba mzazi wa ‘Diamond Platnumz’
TUJIUNGE NA CHANZO
Habari kutoka kwa chanzo makini kilicho karibu na baba Diamond kilidai kwamba kutokana na hali tete ya mzazi huyo ambapo kwa sasa anasumbuliwa na miguu kwa mara nyingine huku ikitoka magamba na kushindwa kutembea kwa muda mrefu, amekuwa akimlaumu mwanaye huyo kupita kiasi.

Diamond Platnumz
Chanzo hicho kilisema kuwa mzazi huyo amekuwa akisema kama alimkosea Diamond, alishamuomba msamaha na akasema amemsamehe lakini hakuonesha mabadiliko yoyote kwake wakati alikiri hadharani kupitia vyombo vya habari. Kiliendelea kueleza kwamba kutokana na jambo hilo baba Diamond amekuwa akiumia kwani mwanaye huyo baada ya kutangaza amemsamehe hajaonesha mabadiliko yoyote ya kumjali.
MALALAMIKO
Chanzo hicho kilidai kwamba, baba Diamond amekuwa akilalamika kuwa ameugua kwa muda mrefu lakini Diamond hajawahi kwenda kumjulia hali hata siku moja.“Ukweli baba Diamond anaumia sana. Sasa hivi anaumwa, ameshindwa hata kutoka nje, miguu imevimba na ina muonekano wa ajabu, amekuwa akisema hajui ni kwa nini mwanaye anashindwa kulegeza moyo wake na kumsamehe wakati alishakiri kwenye vyombo vya habari.“Anasema bora akaenda sasa hivi wakasameheane kuliko asubiri hadi siku akifa ndipo aende,” kiliongeza chanzo hicho.

BOFYA HAPA KUMSIKIA BABA DIAMOND
Baada ya kupata habari hizo, gazeti hili lilitinga nyumbani kwa baba Diamond au Dangote maeneo ya Magomeni-Kagera, Dar na kumkuta akiwa katika hali mbaya kwani miguu imevimba huku ikiwa imepoteza muonekano wa kawaida na kuwa na ngozi ya ajabu.

Baada ya salamu, wanahabari wetu walimuuliza kulikoni yupo katika hali hiyo na kama Diamond alikuwa amekwenda kumjulia hali ambapo alikuwa na haya ya kusema:“Ukweli nimeugua kwa muda mrefu lakini mwanangu Diamond hajawahi kuja kuniona.
AMTUMIA MESEJI
“Hali hiyo ilinifanya juzikati kumwandikia meseji ya kukata tamaa na kumwambia kwamba anaona ameshanizika kutokana na kunisahau kwake lakini Diamond hakunijibu.“Namshukuru Mungu kwa sababu nina kibanda changu cha kulala, silipi kodi kuna watu walishanishauri eti niwatume watu wakaongee naye lakini nilikataa kwa sababu haoni thamani yangu.

ANASUBIRI NIFE?
“Kama ni tofauti na mama yake (Sanura Kassim), tulishamaliza na kabla hajaugua alikuwa anakuja kuniona, nikimuuliza kuhusu Diamond alikuwa akiniambia alishaongea naye lakini kila siku alikuwa akisema atakuja tu kuniona mpaka leo sijamuona labda anasubiri hadi nife ndiyo aje.

“Mara ya mwisho kumuona ilikuwa ni kipindi kile alivyomvisha pete ya uchumba Wema Sepetu ndiyo alimleta kwangu kumtambulisha, tangu hapo huwa namsikia tu kwenye vyombo vya habari. Inauma sana; “Yote kwa yote haya ni maisha tu.”
DIAMOND YUPO BIZE
Ijumaa lilimtafuta Diamond ili kumfikishia habari juu ya baba yake ambapo hakupatikana hewani lakini watu wake wakaribu (Wasafi Classic Baby) walidai kwamba bosi wao huyo alikuwa yupo bize na Zari kwa ajili ya pati yao leo

CHANZO: GPL

No comments:

Post a Comment