Wednesday, November 22, 2017

Dr. Luis Shika kalipwa tena kuuza sura, sasa ni kwenye hii video ya Bongofleva (+video)


Kuna picha zilisambaa juzi kati zikimuonyesha Dr. Luis Shika akiwa na Warembo kwenye kiwanja kimoja cha starehe huku akiwa anakunywa Zanana Juice, sasa imethibitishwa kwamba ile ilikua ni video ya Bongofleva inatengenezwa.
Director Khalfan ambae ndio fundi wa hiyo video ameithibitishia AyoTV na millardayo.com kwamba Dr. Luis Shika amelipwa ili atokee kwenye hiyo video ya Msanii wa Bongofleva ambae alisema hawezi kumtaja kwa sasa.
Hili linakua dili la pili kwa Dr. Luis Shika kulipwa ili kuuza sura ambapo dili la kwanza lilikua ni tangazo la SOKA BET ambako pia alilipwa na kampuni hiyo ilithibitisha kufanya hivyo

Paul Makonda Aibuka Ofisi za Clouds Media Kuwapa Pole


Clouds Wameandika haya Baada ya Paul Makonda Kuwatembelea Kuwapa Pole:
...
"Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam, ikiongozwa na RC Paul Makonda wamefika hapa #Mjengoni - #CloudsMediaGroup kutupa pole na kujionea athari zilizosababishwa na moto uliozuka jana asubuhi katika Ofisi zetu hapa Mikocheni. .
.
Tunashukuru kwa yote, tuko salama"

Picha za Irene Uwoya kwenye kaburi la Ndikumana



Mume wa zamani wa Mwigizaji Irene Uwoya, Hamad Ndikumana alifariki ghafla wiki iliyopita huko Rwanda sekunde chache baada ya kuomba soda ya baridi na kunywa ambapo Irene alifanikiwa kusafiri mpaka kwao kwenda kutoa pole kwa familia.
Kwenye hizi picha hapa chini anaonekana akiwa nyumbani kwa kina Ndikumana na ndugu zake na juu ya kaburi la Ndikumana pia ambapo chini mwishoni kuna video fupi ikimuonyesha Irene akipewa baraka na Baba Mzazi wa Ndikumana
Uwoya akiwa na Familia ya Ndikumana
Baada ya taarifa hizo Irene Uwoya alifunga safari baadae na kwenda kutoa pole kwa familia ya Ndikumana ambapo ameonekana akiwa na Mtoto wao Krissh juu ya kaburi la Ndikumana na kuandika “My trust is in you …R.I.P baba krissh”






Tuesday, November 21, 2017

Isome Hapa Barua ya Kujiuzulu Aliyoandika Rais Robert Mugabe

Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe, Robert Mugabe, jana alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo baada ya kuongoza taifa hilo kwa miaka 37 tangu lilipopata uhuru mwaka 1980.

Mugabe katika barua aliyoiandika kwenda wa Spika wa Bunge, alisema uamuzi huo ni wa kwake binafsi na kwamba hajashinikizwa na mtu yeyote.

Katika barua yake ya kujiuzulu, Mugabe aliiandika jana Novemba 21 na kuielekeza kwa Spika wa Bunge, Jacob Mudenda.

Mugabe aliandika kuwa, kwa mujibu wa kufungu cha 90(1) cha Katiba ya Zimbabwe marekebisho ya namba 20 ya mwaka 2013.

“Kufuatia mazungumzo yangu na Spika wa Bunge, Wakili Jacob Mudenda majira ya saa 7:53 mchana, Novemba 21, 2017 kuhusu kutangaza kujiuzulu kama Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mimi Robert Gabriel Mugabe, kwa mujibu wa kifungu cha 90(1) cha Katiba ya Zimbabwe natangaza rasmi kujiuzulu kwangu kama Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe mara moja.”

“Uamuzi wa kujiuzulu ni wangu kwa chama, na nimefanya hivi kwa maslahi ya watu wa Zimbabwe na nia yangu ya kuona makabidhiano ya madaraka yenye amani ambayo yatashikilia amani, utulivu na umoja wa taifa.”

Aidha, Rais Mugabe alisema, “Tafadhali utangazie umma kuhusu kujiuzulu kwangu haraka iwezekanavyo kama inavyotakiwa na kifungu cha 96(1) cha Katiba ya Jamhuri ya Zimbabwe.

“Wako Mwaminifu, Robert Gabriel Zimbabwe, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe,” alihitimisha Rais Mugabe.

Kufuatia kujiuzulu kwa Mugabe, wananchi katika Mji Mkuu wa Zimbabwe, Harare walitoka katika mitaa mbalimbali na kushangilia huku wakisema kuwa ni awamu mpya kwa Zimbabwe sasa kuendelea kiuchumi.

 

 RIWAYA YA MATESO YA MAMA

Wapendwa Wafuatiliaji wa Blog yetu Kuanzia siku ya Ijumaa ya Tarehe 24/11/2017 Tutawaletea Riwaya ya Mateso ya Mama na itakuwa inendelea kwa kila siku hivyo Mwambie Rafiki,Jirani,na Mtu wako wa karibu kuwa Asikose kufuatilia kwani ni Riwaya nzuri sana.Don't Miss

 

Kutoka kwa Mtunzi wetu Makini RD

MASHINJI ATOA NENO KWA ALIYEKUWA KIONGOZI WA BAVICHA KATAMBI AMBAE SASA AMEHAMIA CCM

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji amesema chama hakina mgogoro na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi ambaye ametangaza kujiunga na CCM kwa kuwa ni haki ya Kikatiba.
 Image result for vicent mashinji
Akizungumza na Mwananchi Jana Jumanne baada ya Katambi kuhamia CCM, Dk Mashinji, “sisi kama chama msimamo wetu tuliuweka tangu madiwani walivyoanza kuondoka, tukaweka msimamo wazi kwamba, suala la mtu kuondoka kwenye chama au kubaki ni suala la Katiba ya nchi ambayo inampa mtu uhuru wa kuhama na kwenda kwenye chama anachotakana.”
Amesema kuwa haoni sababu ya kumzuia mtu kuondoka kwa kuwa mtu anapoamua kwenda sehemu yoyote anakuwa na matarajio.

Pia, Dk Mashinji amesema anamtakia heri (Katambi) na kuwataka CCM kumtumia katika sehemu ambavyo wanaona anafaa kutumika kwa faida ya Watanzania wote.
“Hatuna mgogoro wowote na kimsingi mimi nimtakie tu heri (Katambi) na wakipenda (CCM) wamtumie kwenye eneo watakaloona anafaa kutumika kwa faida ya Watanzania wote,” amesema
Hata Hivyo, Dk Mashinji amesema kuwa walikuwa wanamuandaa Katambi asaidie chama hicho kwenye kitengo cha sheria.
“Alikuwa anamalizia masomo yake ili awe wakili na tulikuwa tumeshaanza kumuandaa ili atusaidie kwenye kitengo cha sheria ndani ya chama,”
Katambi ametangaza leo kujiunga na CCM mbele ya Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) unaofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.