Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa
NIkweli dunia imekwisha! Ni vigumu kuamini mtoto mdogo ambaye anahitaji
uangalizi na ulinzi kutoka kwa jamii anageuzwa mwanamke na kuingiliwa
kwa nguvu hadi mauti. Huu ni unyama na ukatili wa hali ya juu.
Tukio hilo la kutisha lilitokea katikati ya wiki iliyopita, Tabata
Msimbazi jijini Dar ambapo mtoto Ester Banzi ,5, (pichani) alikutwa na
mauti baada ya kuingiliwa kimwili na mwanaume ambaye inadaiwa alimteka
kwanza.
Akizungumza na Gazeti la Uwazi kwenye msiba huo, mama mdogo wa marehemu
Ester aliyejitambulisha kwa jina la Watende Hamis huku akitokwa machozi
mfululizo, alisema:
“Siku ya tukio, ilikuwa saa 5:30 asubuhi tukiwa nyumbani, dada (mama wa
marehemu aitwaye Rebeka) alikuwa ameinjika sufuria ya ugali jikoni kwa
ajili ya chakula cha mchana.
“Akamtuma Ester dukani akanunue unga. Alimpa shilingi 1,200. Si mara ya kwanza Ester kutumwa dukani kwa vile ni jirani tu.
“Tulimsubiri Ester arudi na unga lakini alichukua muda mrefu. Ikabidi
tumfuate dukani, hatukumuona. Tuliwauliza watoto wenzake ambao anapenda
kucheza nao, wakasema walimuona amebeba mfuko cha Rambo huku akiongozana
na baba mmoja.
“Basi, tuliendelea kumtafuta bila mafanikio. Ikabidi tutoe taarifa kwa
baba yake ambaye akaingiwa na wasiwasi, akaenda kutoa taarifa kwenye
Kituo cha Polisi Tabata Shule.“Ndani ya masaa matatu baba yake
akatupigia simu kwamba mwili wa Ester umeokotwa huku ukionekana alibakwa
na kuharibiwa vibaya.”
Naye kijana anayeuza duka ambalo marehemu alitumwa kununua unga, bila
kutaja jina lake alikiri Ester kufika dukani hapo na kupimiwa unga kisha
akaondoka.
Baadhi ya wananchi majirani na maeneo hayo waliohojiwa na waandishi wetu
kuhusiana na tukio hilo walisema kwamba wao walimuona mtoto huyo
akifuatana na mwanamume mmoja, lakini hawakumtilia mashaka kutokana
kwamba walifikiri ni ndugu yao.
Mtu mmoja ambaye mwili wa marehemu ulikutwa jirani na nyumba yake, naye alizungumzia tukio hilo:
“Sisi tulisikia sauti ya mtoto akiomba msaada. Tulipata hofu ikabidi
tukaangalie eneo lile ndipo tulipouona mwili wa mtoto huyo.
Tulipomchunguza tukagundua alibakwa kwani nguo yake ya ndani ilikuwa
pembeni.
“Inaonekana huyo mtu hakuchukua muda mrefu kufanya kitendo hicho.
Tulimpigia simu Mkuu wa Kituo cha Polisi Tabata Shule, Afande Kobelo
akaja na timu yake. Hili tukio nahisi lina ushirikina ndani yake.”
Mmoja wa askari aliyefika katika eneo la tukio ambaye hakutaka kutaja
jina lake kwa vile siyo msemaji mkuu wa jeshi hilo alisema mwili wa
mtoto huyo ulionekana kuingiliwa kimwili, marehemu alivunjwa shingo na
kutobolewa upande wa kushoto kichwani.Marehemu Ester alizikwa wiki
iliyopita mkoani Morogoro. Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya
marehemu. Amina.