Waziri Ummy Mwalimu azindua Duka la Dawa la MSD Kanda ya Mbeya
Na Rabi Hume.
Waziri
wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
amefanya uzinduzi wa duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa Kanda
ya Mbeya.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Waziri Mwalimu amesema uzinduzi wa duka hilo ni
sehemu ya jitihada zinazofanywa na serikali ya Rais Magufuli kuwatia
wananchi huduma bora na kwa gharama nafuu.
“Neema
hii imekuja kwa kipindi cha Rais Magufuli, sasa amekidhi matakwa na
shauku ya wananchi wa Mbeya kwa kuwapa duka la dawa, “Sera ya huduma ya
afya inataka wananchi wachangie isipokuwa wazee, watoto na wajawazito na
kupitia duka hili wananchi wataweza kupata dawa kwa gharama nafuu,”
amesema Mhe. Mwalimu.
Duka hilo la dawa la Kanda ya Mbeya limetumia Shilingi Milioni 13 kwa ukarabati wa jingo na vifaa vyake.
Mh.Ummy
Mwalimu akionesha moja ya dawa inayouzwa dukani hapo kwa shilingi 7,000
ambapo kwenye maduka binafsi inauzwa shilingi 25,000,kushoto ni
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurine Bwanakunu na kulia ni Mfamasia wa duka
hilo, Cornel Mkeng'e.
Mfamasia wa Duka la Dawa, Cornel Mkeng'e akitoa maelezo kwa Mh.Ummy Mwalimu mara baada ya kuzindua duka hilo.
Waziri
wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
akiangalia jinsi ya ufungashaji wa dawa kwenye ghala jipya la Kanda ya
Mbeya.ghala hilo limelozinduliwa leo jijini Mbeya.
Waziri
wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
akipata maelezo jinsi ya utunzaji dawa kwenye ghala hilo.
No comments:
Post a Comment