April 01 2016 Serikali
iliwapandisha kizimbani kamishna wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
‘TRA’ Harry Kitilya, mshindi wa taji la Miss Tanzania 1996 ambaye pia
alikuwa afisa mwandamizi wa benki ya Stanibic tawi la Tanzania Shose
Sinare na Sioi Solomoni kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za kula njama
kutenda kosa pamoja na kosa la kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya
udanganyifu.
Kesi imesikilizwa tena leo
mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es salaam ambapo baada ya
kusikilizwa kwa muda wa takribani masaa matatu, kesi hiyo imeahirishwa
mpaka April 22 itakapotajwa tena na watuhumiwa wamerudishwa rumande.
.
.
.
Harry Kitilya
.
.
.
.
.
.
.
.
Shose Sinare
No comments:
Post a Comment