WAOGELEAJI NANE WA TANZANIA KUSHINDANA KESHO (JUMANNE)
Kocha
wa TSS, Michael Livingstone akiwafundisha waogeleaji Celina Itatiro na
Marin de Villard kwenye bwawa la Ellis Park mjini Johannesburg Afrika
Kusini kwa ajili ya Kusini tayari kushindana katika mashindano ya South
Africa level 2.
Kocha
wa TSS, Alex Mwaipasi akiwafundisha waogeleaji wa TSS, kwenye bwawa la
Ellis Park mjini Johannesburg Afrika Kusini kwa ajili ya Kusini tayari
kushindana katika mashindano ya South Africa level 2
Adil
Bharmal na Pieter De Raadt wakionyesha ufundi wao katika ku-dive wakati
wa mazoezi ya timu ya TSS kwenye bwawa la kuogelea la Ellis Park kabla
ya mashindano ya South Africa level 2
Waogeleaji
wa Tanzania Swim Squad (TFF) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada
ya mazoezi yaliyofanyika kwenye bwawa la Ellis Park mjini Johannesburg
Afrika Kusini tayari kushindana katika mashindano ya South Africa level 2
Viongozi
wa timu ya Tanzania Swim Squad (TSS), Thauriya Diria (wa kwanza
kushoto) na Inviolata Itatiro (Katikati) wakiwa katika picha ya pamoja
na kocha Michael Livingstone wakiwa katika picha ya pamoja TSS kwenye
bwawa la kuogelea la Ellis Park kabla ya mashindano ya South Africa
level 2
………………………………..
Na Mwandishi wetu,Johhanesburg
Jumla
ya waogelaji nane wa timu ya Tanzania Swim Squad (TSS) watakuwa na
ratiba ngumu kesho ya kuwania medali mbalimbali katika siku ya pili ya
mashindano ya Kimataifa ya Afrika Kusini “South Africa Level 2”
yaliyoanza jana kwenye bwawa la kuogelea la Ellis Park.
Waogeleaji
hao ni Celina Itatiro, Marin de Villard, Adil Bharmal, Amani Dogart,
Josephine Oosterhuis, Jacquelene Kortland, Isabella Kortland, Pieter De
Raadt, Celina Itatiro na Marin de Villard.
Waogeleaji
hao watawania medali katika mashindano ya mita 50, 100, 200 na relay
katika kwa upande wa wanawake na wanaume kwa kushindana na waogeeaji
wengine kutoka nchi za Zimbabwe, Msumbiji, Namibia na wenyeji Afrika
Kusini.
Kwa
mujibu wa ratiba iliyotolewa na waandaaji, Adil ndiye ataanza kuwania
medali kwa uande wa Tanzania kwa waogeaji wenye umri miaka 16 na
kufuatiwa na Marin kwa upande wa mita 200 freestyle kwa waogeleaji wa wa
miaka 11 na baadaye wasichana, Celina na Amani kushindana kwa upande wa
wanawake wenye umri wa miaka 11 katika staili ya free style.
Ratiba
hiyo inaonyesha kuwa Adil na Marin wataingia tena kwenye ‘maji’
kushindana katika staili ya breaststroke mita 100 kwa upande wa umri wao
ns baadaye Josephine na Jacqueline watapambana kwa watoto wenye umri wa
miaka 15 na kufuatiwa na Celina na Amani tena.
Baada
ya kushindana katika staili hizo mbili (freestyle na breaststroke mita
100 na 200), waogealeaji, Adil na Marin wataingia tena mashindananoni
kuwania medali kwa upende wa mita 50 backstroke na baadaye Isabela
Kortland, Josephine, Amani na Celina watawania medali tena.
“Ni
ratiba ngumu sana kwa waoageaji wetu, ila tunashukuru kuwa wameweza
kufanya mazoezi na kidogo kuzoea hali ya hewa ya ubaridi, sisi (TSS)
tutatokea mji wa joto inaweza kutupa shida kwani baridi ya huku
inaambatana na jua la kuchoma, si hai nzuri, ila tutajitahidi,” alisema
Alex Mwaipasi.
Mwaipasi
ambaye yupo na kocha mwenzake, Michael Livingstone alisema kuwa
mashindai hayo ni magumu sana kutokana na idadi ya waogeleaji na idadi
ya mashindano ambayo kila muogeleaji atashindana.
“Celina
anatarajia kushindana katika mashindano tofauti 11, si mchezo na
waogeleaji wpo zaidi ya 1000, nchi nyingi za ukanda wa Kusini mwa Afrika
wameleta waogeaji, ni mashindano mazuri kwa kuwapa uzoefu waogeleaji
wetu,” alisema Michael.
No comments:
Post a Comment