Wachimbaji wadogo Geita Watakiwa kuvuta subira
Afisa
Madini Mkoa wa Geita Fabiani Mshai amewataka wachimbaji wadogo wadogo
Mkoani humo kuwa wavumilivu wakati Ofisi yake kwa kushirikina Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa huo wakitafuta maeneo ya kumwaigia mawe yanayodhaniwa
kuwa dhahabu maarufu kwa jina la magwangala.
Akizungumza
na channel Ten kuhusu maeneo ya kumwaga mawe hayo kama walivyoagizwa
na waziri mkuu amesema si kwamba Serikali imekaa kimya bali utaratibu
unaendelea wa kupata maeneo yaliyo salama.
Amesema
maeneo yote ambayo hayakumilkiwa na watu wameyachukua na utafiti
unafanyika ili kubaini kama kuna dhahabu ili waweze kuwapa maeneo hayo
wachimbaji wadogo.
Juzi
wachimbaji wa Mgusu walifanya mkutano baada ya eneo lao kufungwa na
kubainisha maeneo ambayo Serikali ikiwapatia wanaweza kupata riziki na
familia zao na hapa wanayabanisha.
No comments:
Post a Comment